Makamu wa Rais kufungua Mkutano Mkuu wa ALAT Arusha

NA PETER JOSEPH

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kesho atakuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) utakaofanyika katika Ukumbi wa Simba AICC jijini Arusha. 
Mkutano huo utakaofanyika kuanzia Mei 29, 2023 na kukamilika tarehe 31 Mei, 2023 utawakutanisha washiriki 600, wakiwemo Wastahiki Mameya wa Majiji na Manispaa, Waheshimiwa Wenyeviti wa Halmashauri, na Wakurugenzi wa Halmashauri zote 184 za Tanzania Bara. 

Katibu Mkuu wa ALAT Taifa Bw. Mohamed Maje amesema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya kufanyika kwa mkutano huo yamekamilika. 

Wakati huo huo, Benki ya NMB leo tarehe 28 Mei, 2023, imekabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya kufanikisha Mkutano Mkuu wa 37 wa ALAT. 
Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa na Viongozi wa ALAT Taaifa wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe. Sima Constantine Sima, Katibu Mkuu wa ALAT Bw. Mohamed Maje, na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Tendaji wa Jumuiya hiyo. 

Akizungumza kabla ya kupokea hundi hiyo, Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe. Sima Constantine Sima ameishukuru Benki ya NMB kwa kushirikiana na Jumuiya hiyo kwa muda wa miaka saba.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB Bw. Alfred Shao ambaye alimwakilisha Mtendaji Mkuu wa NMB amesema Benki hiyo na ALAT wamekuwa wakishirikiana pamoja katika kuboresha miundombinu ya Elimu, Afya, Usafiri na Mazingira kupitia halmashauri 184 nchini.
Amesema Benki ya NMB imeendelea kuboresha huduma zake ili kuweza kuhudumia Serikali Kuu pamoja na Serikali za Mitaa. 

Ameongeza kuwa kazi kubwa ya Benki hiyo ni ni kurahisisha makusanyo ya kodi kupitia mifumo bora inayowezesha Serikali ya awamu yaa ssita katika makusanyo ya mapato. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news