NEMC, BASATA ana kwa ana na wadau wote wa muziki,sherehe Dar

NA GODFREY NNKO

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wameandaa Mkutano juu ya Udhibiti wa Kelele na Mitetemo kwa wamiliki wa baa, kumbi za sherehe na burudani au starehe,bendi, wasanii, wakuzaji wa sanaa (promotors), waendesha vyombo vya muziki (DJs),waongoza sherehe (MCs) na wadau wengine wa muziki.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 14, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira,Dkt.Mhandisi Samuel Gwamaka Mafwenga ambapo mkutano huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Mei 17, 2023.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, lengo la mkutano huo ni kukuza uelewa juu ya matakwa ya Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Viwango vya Udhibiti wa Kelele na Mitetemo) za mwaka 2015.

Aidha,mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa ni Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, CPA Amosi G.Makalla.

"Hivyo, wadau wote mnaalikwa kushiriki mkutano huu muhimu utakaotoa fursa ya kuainisha changamoto mbalimbali na kutoa maoni juu ya namna bora ya kuimarisha Uzingatiaji wa Kanuni na Viwango vya Kelele na Mitetemo bila kuathiri Uzingatiaji wa Sheria na Kanuni za viwango vya Kelele na Mitetemo pamoja na uendeshaji bora wa shughuli za sanaa nchini,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news