Raia wa Marekani ahukumiwa jela miaka 20 kwa kukutwa na dawa za kulevya Dar es Salaam

NA DIRAMAKINI

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imemuhukumu, Lione Lionel Rayford raia wa Marekani kifungo cha miaka 20 jela.
Ni baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin kiasi cha kilo 2.188. 

Hukumu hiyo imetolewa Mei 26, 2023 kufuatia Shauri la Uhujumu Uchumi namba 17 la mwaka 2021 lililokuwa mbele ya Mheshimwa Jaji Isaya kumalizika pasipo shaka kwamba, mshtakiwa alijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya. 

Mtiwa hatiani alikamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) tarehe 5 Julai, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa ameficha dawa hizo katika moja ya mabegi aliyokuwa nayo.

#kataadawazakulevya_timizamalengoyako 

#dawazakulevyanihatari

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news