Rais Dkt.Mwinyi akabidhiwa Ripoti ya CAG

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ikulu jijini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akipokea Ripoti ya Mwaka 2022-2023 ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Dkt.Othman Abbas Ali (katikati) Mei 11, 2023 Ikulu jijini Zanzibar. Anayeshuhudia katika hafla hiyo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora, Mhe.Haroun Ali Suleiman. (Picha na Ikulu).

Akipokea ripoti hiyo, Rais Dkt.Mwinyi amemuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora kuiwasilisha katika Baraza la Wawakilishi.

Akizungumza baada ya kukabidhi riporti hiyo kwa Rais Dkt.Mwinyi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Dkt.Othman Abass Ali alisema wamewasilisha ripoti saba ikiwemo ya Serikali Kuu (Wizara na taasisi zote), Mashirika na Taasisi zinazojitegemea.

Pia ripoti ya Idara Maalum na taasisi zake, ripoti ya mifumo yote ya Tehema ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ripoti ya mashirika ya umma, na ripoti ya ufanisi ya miradi ya maendeleo iliyofadhiliwa na fedha za Uviko 19.

Alisema, ripoti hizo zipo za aina mbili ikiwemo miradi ya maendeleo ya wahisani pamoja na ya Serikali pamoja na ripoti za kiufundi.

“Tunapojenga tunatakiwa kufanya ukaguzi wa thamani ye fedha, tumefanya ukaguzi huu kwa sekta za Afya na Elimu kwa skuli zote 12 zilizojengwa," alieleza CAG.

Pia alieleza walifanya ukaguzi kwa skuli ya Bweleo ambayo Serikali iliinunua na skuli zote zilizofanyiwa matengenezo ikiwemo vyoo vya skuli hizo na kuonesha yote yaliyobainika kwenye ukaguzi huo.Kifungu cha 112 (5) kinamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali awasilishe taarifa yote aliyoikagua na aikabidhi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa hatua nyingine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news