Rais Dkt.Mwinyi akabidhiwa ripoti ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema kupitia takwimu zilizotolewa na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Serikali ina jukumu la kujipanga kwa utekelezaji wa kiuchumi na kijamii.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla (wa tatu kushoto) alipokuwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Ripoti ya Sensa ya mwaka 2022 leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Ameyasema hayo leo Ikulu jijini Zanzibar katika hafla fupi ya kukabidhiwa ripoti ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 iliyofanywa na Makamu mwenza wa Kamati ya Ushauri wa Sensa kitaifa , Makamu Pili wa Rais Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdullah na ujumbe wake .

Matokeo ya takwimu hizo yameonesha kwamba ongezeko la idadi la Watu Zanzibar imefikia asilimia 3.7 kwa Mwaka.

Vilevile ifikapo mwaka 2025 kuhitimisha Dira ya Maendeleo ya Tanzania, Zanzibar itakuwa na idadi ya Watu wapatao milioni 2.08 , Dunia itakapohitimisha malengo endelevu mwaka 2030 Zanzibar inakadiriwa idadi ya watu itakuwa milioni 2.44 , na mwisho wa Dira 2050 Zanzibar inakisiwa kuwa na idadi ya watu Milioni 4.63.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news