Rais Dkt.Mwinyi awakaribisha wawekezaji kutoka nchini Qatar

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi baada ya kuwasili jana usiku jijini Doha, Qatar akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano mkubwa wa Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi utakaofunguliwa kesho amewakaribisha wawekezaji kutoka Qatar kuja kuwekeza nchini.

Katika ziara yake Rais Dkt. Mwinyi leo asubuhi amekutana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Qatar, Mhe. Muhamed Bin Ahmed Al-Kuwari na wadau kutoka sekta binafsi ya viwanda.
Rais Dkt. Mwinyi amewakaribisha wafanyabiashara hao wakubwa kuwekeza Zanzibar kutokana na fursa zilizopo pia aligusia eneo jipya la uwekezaji ambalo ni utalii wa kumbi za mikutano.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa ZIPA, Shariff Ali Shariff alieleza umuhimu wa kukutana kwa mabaraza ya uwekezaji ya Zanzibar na Qatar ili kuimarisha uhusiano zaidi.

Pia alielezea fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar zaidi kwa upande wa utalii kwani ujenzi wa hoteli kubwa za kifahari unahitajika kutokana na soko la utalii kuongezeka.

Fursa nyingine alizowakaribisha kuwekeza ni ukodishaji wa visiwa vidogo.

Halikadhalika aliwafahamisha kwa undani fursa zilizopo katika sera ya uchumi wa Buluu ambayo imewagusa zaidi wawekezaji hao hasa suala la uchimbaji wa gesi na mafuta.

Eneo jingine ni shamba la Makurunge Bagamoyo ambalo ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar linalofaa kwa utalii na hata kilimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news