Nelson Memorial Secondary School yawa kivutio Dodoma

DODOMA-Nelson Memorial Secondary School iliyopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma imeendelea kuwa kivutio kwa wazazi na walezi wengi kutokana na namna ambavyo imekuwa ikitoa huduma bora kuanzia elimu, malezi na maadili.
Shule hiyo ambayo ina usajili Na.S5879 ambayo ni ya bweni kwa wavulana na wasichana kipaumbele chao ni nidhamu na taaluma. 

Kwa nyakati tofauti, baadhi ya wazazi wamesema, chaguo lao la kwanza limekuwa shule hiyo kutokana na namna ambavyo watoto wao wanafundishwa vema huku malezi ya kiimani na maadili yakiwa ndiyo msingi wao.

"Sijutii kumleta mwanangu hapa Shule ya Sekondari Nelson Memorial, kwangu ni chaguo la kwanza na ninaamini nilifanya uamuzi sahihi kabisa wa kumleta mwanangu hapa.
"Hii ni shule nzuri ambayo licha ya kipaumbele kuwa nidhamu na taaluma pia watoto wanalelewa katika misingi bora ya kiimani na maadili,"amesema mmoja wa wazazi shule hapo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news