Tanzania yajifunza namna ya kutunza historia kupitia sanaa

NA ELEUTERI MANGI
Cape Town, Afrika Kusini

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema katika ziara yao ya kikazi mji wa Century, Cape Town Afrika Kusini leo Mei 27, 2023 wamejifunza namna ya kutunza historia kupitia sanaa.
“Sanamu hizi zinauwezo wa kudumu kwa muda mrefu zaidi na kuwa kumbukumbu nzuri kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo na kuwafanya waonje na kujua nchi yao imetoka wapi, ipo wapi na wanakwenda wapi hatua ambayo inatoa fundisho na kutumia historia hiyo kuinua maisha ya watu na uchumi wa nchi,”amesema Bw. Yakubu. 
Katika ziara hiyo, yupo pia Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Bi Fatma Hamad Rajab ambao wamefika “The Long March to Freedom” kujifunza namna sanamu za shaba zinavyosadifu maisha mashujaa wa kupigania uhuru kila mmoja kwa aina yake na hazipatikani sehemu nyingine zaidi ya mji wa Century City huko Cape Town Afrika Kusini.
Miongoni mwa sanamu za kumbukumbu za mashujaa hao ipo pia ya Baba wa Taifa la Tanzania Mwl. Julius Kambarage Nyerere (1922-1999) akiwa ameorodheshwa namba kumi na mbili (12) karibu na sanamu ya namba 11 ya Helen Suzman (1917-2009) na kwa upande mwingine ipo sanamu ya namba 13 ya Fidel Castro namba (1926-1916) na viongozi wengine ambao huvuta hisia za watu wanaofika kutembelea eneo hilo ambalo ni adhimu ya ukombozi wa nchi za Afrika.
Sanamu nyingine ambazo zipo katika makumbusho hayo ni ya Walter Sisulu (1912-2003), Nelson Mandela (1918-2013), Samora Machel (1933-1986), Oliver Tambo (1917-1993), Solomon Mahlangu (1956-1979), Mohandas “Mahatma-Gandhi (1869-1948), Dkt. Martine Luther King JR (1929-1968), Archbishop Emeritus Desmond Tutu (1931-2021) pamoja na wengine wengi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news