Wafanyakazi wahujumu Shirika la Umeme la Afrika Kusini (Eskom)

NA DIRAMAKINI

MFANYAKAZI wa zamani wa kandarasi ya muda mfupi ya Shirika la Umeme la Afrika Kusini (Eskom) katika Kituo cha Umeme cha Tutuka amekamatwa Mei 10,2023 kwa ulaghai na ufisadi.
Muonekano wa Kituo cha Umeme cha Tutuka huko Standerton, Afrika Kusini.(Picha na Gallo/Rapport/Deon Raath).

Zandile Rosemary Ngcobo, ambaye aliajiriwa kama Afisa Manunuzi, alifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Standerton siku hiyo hiyo na kuachiliwa kwa dhamana ya Randi 5,000.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kushirikiana na wafanyakazi wawili wa Eskom na msambazaji bidhaa katika kununua kontena la usafirishaji kwa bei iliyoongezwa ya Randi 939,550. Kontena hilo liliwasilishwa kwenye tovuti, hata hivyo, halikukidhi masharti na lilikuwa na thamani ya Randi 20,000 pekee.

Matokeo yake, Eskom ilipata hasara ya Randi 919,550. Ngcobo alionekana tena pamoja na mshtakiwa mwenzake Jessie Phindile Kubeka, ambaye ni mbia wa kampuni ya wasambazaji wa Eskom iitwayo Mnandi (Pty) Ltd, wafanyakazi wa Eskom Sarah Nomsa Sibiya, Fundi Mwandamizi wa Uendeshaji na Bhekizizwe Solomon Twala, Mfanyabiashara Mwandamizi, ambao wote wanakabiliwa na kesi hiyo ikiwa ni mashtaka sawa katika Mahakama ya Uhalifu wa Kibiashara ya Middleburg mnamo Mei 11, 2023.

Kw amujibu wa Business Tech, watuhumiwa hao watafikishwa tena katika Mahakama ya Biashara ya Middleburg Juni 8, 2023.

"Eskom itaendelea kutoa msaada unaohitajika kwa Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini (SAPS) na Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka (NPA) ili kuhakikisha kuwa washukiwa wanashitakiwa kwa mafanikio na kwamba adhabu kali inatolewa kama matokeo mazuri ambayo yatatumika wazuie wahalifu wengine.

"Kukamatwa huku kunaendelea kudhihirisha harakati za Eskom kuhakikisha kuwa wahalifu wanakabiliwa na nguvu kamili ya sheria na kutovumilia uhalifu,"Business Tech iliripoti.

Aidha, kukamatwa huko kunafuatia msururu wa operesheni zilizofanikiwa ambapo wafanyakazi wa Eskom, wakandarasi na wasambazaji wameendelea kubanwa kwa kulaghai shirika hilo la umeme.

Mnamo Aprili, wafanyakazi watatu wa Eskom walikamatwa kwa kuhusika katika wizi wa makaa ya mawe. Wafanyakazi wengine walikamatwa kuhusiana na wizi wa dizeli, hujuma na uhalifu mwingine uliopangwa katika shirika hilo.

Imekuwa jambo la kawaida kuwa makundi ya wahalifu yanafanya kazi ndani na nje ya Eskom, huku Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Eskom, Andre de Ruyter akidai kuwa wanasiasa wa ngazi za juu wanahusika.

Katika ripoti iliyochapishwa mwezi huu, De Ruyter alisema kuwa kumekuwa na matukio ambapo malori ya makaa ya mawe yamesimamishwa kwenye vizuizi vya barabarani kwa ukaguzi na maafisa wanaosimamia walipokea simu kutoka ngazi za juu wakiwaambia waondoke.

Mtendaji huyo hajataja hata mmoja wa wanasiasa wanaodaiwa kuhusika, lakini ameelekeza lawama kwa Waziri wa Mashirika ya Umma, Pravin Gordhan kuwa anawajua ni nani na pia hashangazwi ha hali hiyo.(Business Tech)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news