Wafutwa kazi kwa ubadhirifu vijijini

NA DIRAMAKINI

PASCHAL Thayo ambaye ni afisa mtendaji wa Kijiji cha Sabilo kilichopo Kata ya Dabil na Hussein Rashid ambaye ni mtendaji wa Kijiji cha Kimara kilichopo Kata ya Kiru ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara wamefukuzwa kazi.

Uamuzi huo umefikiwa na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara kwa kudaiwa kufanya ubadhirifu wa fedha za umma na utendaji kazi mbovu.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Anna Mbogo wakati akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika katika makao makuu yao yaliyopo Kata ya Ari.

Mbogo amesema, uamuzi wa kuwafuta kazi maofisa watendaji hao wa vijiji ni kufuatia uchunguzi uliofanywa na madiwani na kubainika kufanya ubadhirifu hivyo kutoridhishwa na utendaji kazi wao.

"Uamuzi huu ni kufuatia uchunguzi uliofanywa na madiwani wa halmashauri na kubaini ubadhirifu na kutoridhishwa na utendaji kazi wa watumishi hao wawili," amesema Mbogo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, John Noya amewataka watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipavyo na kuwahudumia wananchi, kwani wakifanya makosa ya kujitakia na ubadhirifu watawachukulia hatua kali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news