Waziri Mhagama awataka wakandarasi ujenzi Mji wa Serikali Mtumba kuongeza kasi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, amewataka wakandarasi wanaondelea ya shughuli ya ujenzi wa majengo ya Mji wa Serikali Mtumba Dodoma kuongeza kasi, na kufanya vikao vya mara kwa mara ili kuweza kutatua changamoto za ujenzi wanazokutana nazo. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na timu aliyoambatana nayo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa majengo ya ofisi za Serikali Mtumba Dodoma, ziara ilifanyika tarehe 6 Mei, 2023.

Waziri Mhagama ameyasema hayo leo Mei 6, 2023 alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa baadhi ya majengo hayo na kuwaasa wakandarasi hao kujenga majengo yanayoendana na thamani ya fedha zilizopangwa na kuhepuka ucheleweshwaji ili kufikia malengo ya Serikali. 

“Fanyeni kazi kwa pamoja na kuhakikisha mnaongeza kasi ya ujenzi, muwe na site meetings, tatueni changamoto kwa wakati, thamani ya fedha ilingane na mradi na thamani ya mradi iendane na fedha, hatuhitaji kuwa na delays yoyote katika ujenzi wa mradi huu,”alisema Mhe. Mhagma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na timu aliyoongozana nayo wakikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii Mjumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na timu aliyoongozana nayo wakikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii Mjumba jijini Dodoma.
Mratibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Serikali Kuhamia Dodoma na Msimamizi wa ujenzi wa Mji wa Serikali Bw. Meshack Bandawe akifafanua jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake Mji wa Serikali Mtumba.
Mhandisi kutoka NHC, Grace Musita akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama muonekano wa ramani ya jengo la Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mtumba Dodoma.
Alipokuwa katika Jengo la Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, aliwaasa Wakandarasi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutumia fursa ya ujenzi wa Mji wa Serikali kwa kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kuuza ujuzi kwa wageni watakaotembelea mji huo wa Serikali mbeleni na kuwawezesha kuteka soko la Nchi za Afrika Mashariki na nchi za kusini mwa Afrika. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Shirika la Nyumba la Taifa NHC Mhandisi Aikani Mlekeo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.

Kwa Upande wake Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara hiyo kutoka Shirika la Nyumba la Taifa NHC Mhandisi Aikani Mlekeo Alisema “ Tunaishukuru Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu chini ya Usimamizi wa mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Bw. Mesharck Bandawe, kwa kutupa Mwongozo mzuri katika usimamizi wa Ujenzi wa Mradi huu.” 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akikagua ujenzi unaoendelea wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU). 

Ziara hiyo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, ilihusisha kutembelea na kukagua baadhi ya ujenzi wa majengo ya Serikali ikiwa ni pamoja Eneo la ujenzi wa Mradi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu na Eneo linalojengwa Uwanja wa Mashujaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news