Zamaradi Mketema azindua rasmi Zamaradi TV inapatikana Azam TV chaneli namba 413

NA DIRAMAKINI

HATIMAYE Chaneli ya Habari, Burudani na Mtindo wa Maisha ambayo ina aina ya programu mbalimbali ikijumuisha misururu ya vipindi vya maongezi na majadiliano ya Zamaradi TV imezinduliwa rasmi.

Uzinduzi huo umefanyika Mei 2,2023 jijini Dar es Salaam chini ya mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu, Bi. Zamaradi Mketema.
Kwa sasa Zamaradi TV itapatika katika king'amuzi cha Azam TV cha dishi katika chaneli namba 413.

Bi.Zamaradi amesema, alikuwa kimya kwa muda mrefu za shughuli nyingi zilisimama katika kuhakikisha ndoto ya kuzindua chaneli hiyo inakamilika

“Sababu kubwa ya kuchelewa ni kwamba tulizindua online TV na tukatangaza kuwa tutazindua TV na tulitamani jambo hili lisiwe na mkono wa mtu, tusimamie sisi wenyewe,”amesema Zamaradi.

Ameongeza kuwa, fundisho kubwa alilolipata katika ndoto yake ni kwamba hakuna kitu kwa ajili ya mtu fulani, badala yake kila kitu ni kwa ajili ya kila mtu.

“Ningeweza kukata tamaa na kuona kuwa hii ni ya watu fulani, lakini nimepigana na kuhakikisha nimefika hapa nilipofika leo, maneno ni mengi ya kukatisha tamaa na kama una roho ndogo unaweza kukata tamaa katika kutimiza ndoto yako,” amesema.

Yeye ni nani?

Zamaradi Mketema alizaliwa tarehe 4 Oktoba mwaka 1985 jijini Dar es Salaam.Ni mtangazaji wa redio na televisheni kutoka Tanzania aliyepata umaarufu kwa utangazaji wake kwenye kipindi cha Take One kilichokuwa kikirushwa na kituo cha televisheni cha Clouds.

Zamaradi Mketema alianza kuwa mtangazaji kwenye kituo cha Televisheni cha C2C kati ya mwaka 2007 hadi 2008.

Mbali na utangazaji pia alitoa filamu ya kwanza iliyoitwa Nzowa, kisha mwaka 2014 alifanikiwa kutoa filamu yake ya Kigodoro aliyowashirikisha wasanii wengi wa Tanzania na kufanikiwa kushinda kwenye tuzo za watu kama filamu bora ya mwaka, lakini pia alitengeneza documentary inayofahamika kama neno la mwisho inayohusu maisha ya marehemu Steven Kanumba ambayealikuwa muigizaji mkubwa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news