Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Juni 29,2023
Serikali imesema imefanya jitihada kubwa ya kupunguza changamoto za biashara nchini hususani kupunguza utitiri wa tozo kutoka 380 hadi 148 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 hadi 2020/2021.Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande ameyasema hayo Juni 28, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Buhigwe, Kavejuru Felix (CCM).