Katibu Mkuu Yakubu asisitiza ubunifu sekta ya sanaa

NA ELEUTERI MANGI-WUSM

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw.Saidi Yakubu amewasisitiza watendaji na watumishi wa taasisi chini ya wizara hiyo kuwahudumia wadau wa sekta ya Utamaduni na Sanaa kwa wakati ili kuleta tija katika utendaji kazi.
Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema hayo leo Juni 20, 2023 jijini Dar es Salaaam alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania pamoja na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania.

"Tuongeze ubunifu zaidi na kurasimisha wafanyabiashara wa kazi za Utamaduni na Sanaa na wasanii ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma kwa wadau wa sekta zetu hizi," amesema Bw. Yakubu.
Ameongeza kuwa, taasisi zote za wizara zina wajibu kutekeleza vipaumbele vya Serikali ikiwemo kuongeza wigo wa wasanii kwenda kufanya kazi za sanaa nje ya nchi na kutangaza Utamaduni na Sanaa ya Tanzania na kuongeza ubunifu katika utendaji kazi wao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news