TANZIA:Adolph Nicholas Mbinga mpiga solo mahiri afariki

NA DIRAMAKINI

MPIGA solo mahiri nchini,Adolph Nicholas Mbinga amefariki dunia kijijini kwao Mpute katika Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoifikia DIRAMAKINI, imedaiwa ugonjwa ambao ulikuwa unamkabili ulimzidi ikiwa ni siku chache kabla ya kuacha kula kabisa.

"Ndugu yetu na mwanamuziki mwenzetu Adolph Nicholas Mbinga mpiga solo mahiri ametangulia mbele ya haki.

"Amefariki majira ya saa 5:30 usiku wa Alhamisi ya Juni 15, 2023.Amefia kijijini kwao Mpute Wilaya ya Nachingwea.

"Ugonjwa ulimzidia, pia siku chache hizi za mwisho aliacha kula kabisa.Mipango ya mazishi tutajulishana.Tulimpenda, lakini Mungu amependa zaidi,Mwendo ameumaliza, kilichobaki tumuombee mapumziko ya amani,"kimeeleza chanzo cha taarifa iliyofikia DIRAMAKINI.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news