Waziri Kairuki aishukuru Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson

NA JAMES MWANAMYOTO 
OR-TAMISEMI 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Angellah Kairuki ameishukuru Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson (Henry Jackson Foundation for Medical Research International) kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson, Meja Jenerali mstaafu, Dkt. Joseph Caravalho wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha viongozi hao. 

Mhe. Kairuki ametoa pongezi hizo Juni 20, 2023 kwa Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson, Meja Jenerali mstaafu Dkt. Joseph Caravalho aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dodoma. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson, Meja Jenerali Mstaafu Dkt. Joseph Caravalho ambaye taasisi yake inatoa mchango katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Mhe. Kairuki amesema, Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Tanzania inadhibiti janga la UKIMWI kupitia kinga, matunzo, matibabu ya VVU na utoaji wa msaada kwa watu wanaoishi na VVU. 
Mhe. Kairuki amefafanua kuwa, taasisi hiyo ya utafiti maarufu kama Walter Reed Program imekuwa ikifanya kazi kwa miaka mingi tangu mwaka 2004 akitoa mfano kwenye mikoa ya nyanda za juu kusini ambayo ni Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi na Ruvuma ambapo taasisi hiyo imeshirikiana vema na Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Paul Chaote (wa kwanza kulia) akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki wakati wa kikao kazi chake na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson, Meja Jenerali Mstaafu Dkt. Joseph Caravalho ambaye taasisi yake inatoa mchango katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Naye, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson, Meja Jenerali mstaafu wa Jeshi la Marekani, Dkt. Joseph Caravalho ameishukuru Serikali ya Tanzania chini ya uongozi makini wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa ni kinara wa kujenga mahusiano ya kidplomasia yaliyoiwezesha taasisi yake kutoa mchango katika eneo la mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news