Waziri Mchengerwa afanya uteuzi NCT na NCAA

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa (Mb) amefanya uteuzi wa watendaji wawili kushika nafasi mbalimbali kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 14, 2023 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kupitia wizara hiyo, John Mapepele ambapo amefafanua kuwa, kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hassan Ababasi uteuzi huo unaanza leo.

"Kwanza, Mheshimiwa Waziri amemteua, Dkt.Florian Geofrey Mtey kuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), uteuzi huo ni kwa mujibu wa Amri ya uanzishwaji wa Wakala wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) ya mwaka 2003, Kifungu cha 2.2.

"Pili, Mheshimiwa Waziri, amemteua Kamishna Msaidizi, Salim Athuman Mjema kukaimu nafasi ya Naibu Kamishna wa Huduma za Shirika kwenye Mamlka aya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), nafasi iliyoachwa wazi na Needpeace Wambuya aliyehamishwa kituo kingine cha kazi,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo ni kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (3) cha Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Sura ya 284 kama ilivyoboreshwa mwaka 2002.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news