Wanavijiji mbioni kuanza kutumia maji ya bomba

NA FRESHA KINASA

VIJIJI mbalimbali katika Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara vimeendelea kuneemeka kupitia miradi ya maendeleo ikiwemo ya maji.
Aidha,kata nne zenye jumla ya vijiji 12 za Jimbo la Musoma Vijijini zina miradi ya kusambaziwa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria.
Ujenzi umeanza tokea wiki iliyopita na Mbunge wa jimbo, Prof. Sospeter Muhongo alienda kukagua ujenzi huo ambapo mradi wa bomba kuu la maji la Mugango-Kiabakari-Butiama unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 70.5.
Kupitia mradi huo unatarajiwa kuzalisha zaidi ya maji lita milioni 35 kwa siku ambapo mitambo ya kusukuma maji inayotengenezwa China, Hungary na Turkey italetwa nchini hivi karibuni.
Pia, ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kutoka bomba kuu la Mugango-Kiabakari-Butiama utafika kata za Tegeruka na Mugango huku ukitarajiwa kugharimu shilingi bilioni 4.75.
Wakati huo huo, mitaro ya urefu wa takribani kilomita 15 tayari imechimbwa na bomba zitaanza kutandazwa hivi karibuni.
"Tenki lenye ujazo wa lita 135,000 linajengwa kijijini Kataryo. Hili tenki litapokea maji kutoka kwenye tenki la kijijini Kiabakari lenye ujazo wa lita milioni tatu. Aidha,kata za Busambara na Kiriba tenki la ujazo wa lita 500,000 limejengwa kwenye Mlima wa Kong'u kijijini Kwibara, Kata ya Mugango.

"Vijiji sita vya kata za Busambara na Kiriba vitapata maji ya bomba kutoka kwenye tenki hili.Miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye kata hizi mbili itaanza kujengwa, hivi karibuni, Agosti 2023
"Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji ya bomba vijijini mwetu. Kila kijiji kinao mradi wa maji. Asante sana,"imefafanua sehemu ya taarifa kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.
Picha zilizoambatanishwa zinamuonesha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijinini, Prof. Sospeter Muhongo akiongea na wananchi wa vijiji vitatu (Tegeruka, Mayani na Kataryo) vya Kata ya Tegeruka. 

Hiyo ilikuwa siku ya Jumapili, Juni 11, 2023 wakati Mbunge huyo alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye vijiji hivyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news