AU watoa siku 15 kwa utawala wa kijeshi Niger

ADDIS ABABA-Umoja wa Afrika (AU) umetoa siku 15 kwa utawala wa kijeshi nchini Niger kusimamisha tena Serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na kumruhusu Rais Mohamed Bazoum kuanza tena majukumu yake.
Taarifa ya Baraza la Amani na Usalama la AU ilimeeleza kuwa, umoja huo unasikitishwa na kuzuka tena na hali ya kutisha ya mapinduzi ambayo yanadhoofisha demokrasia na utulivu katika bara la Afrika.

Pia, imewataka askari hao kurejea mara moja na bila masharti kwenye ngome zao na kurejesha mamlaka ya kikatiba, ndani ya muda usiozidi siku kumi na tano.

Rais Bazoum ambaye hali yake na ya maafisa wake bado haijajulikana tangu serikali ilipopinduliwa, taarifa hiyo imebainisha kuwa wanapaswa pia kuachiliwa mara moja na bila masharti.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kushindwa kufanya hivyo kutalazimisha umoja huo kuchukua hatua za lazima, ikiwa ni pamoja na hatua za adhabu dhidi ya wahusika.

Awali, Jenerali Abdourahmane Tchiani alitangaza katika Televisheni ya Taifa kuondolewa kwa Rais Bazoum madarakani, amri ya kutotoka nje na kufungwa kwa mipaka.

Vile vile Jumatano iliyopita, Rais Bazoum alizuiliwa na baadhi ya wanachama wa walinzi wa rais katika mji mkuu, Niamey.

Kati ya 2020 hadi sasa, Afrika imekuwa na visa 10 vya mapinduzi ya serikali viilivyokamilishwa au kudhibitiwa ambapo nchi zilizoathirika ni pamoja na Sudan, Chad, Burkina Faso, Mali, Guinea, Guinea-Bissau, na kwa sasa Jamhuri ya Niger.(Mashirika/DIRAMAKINI).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news