DC Mkasaba awashukuru Wanadaispora

ZANZIBAR-Wanadaispora kutoka nchini Marekani wamepongezwa kwa juhudi zao za kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha huduma ya afya kwa jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Rajab Yussuf Mkasaba ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea Kambi ya Wanadiaspora hao wakiwemo madaktari bingwa waliokuwa wakitoa huduma za afya kwa wananchi huko katika Hospitali ya Wilaya ya iliyopo Kitogani, Wilaya ya Kusini Unguja.

Katika maelezo yake, Mkasaba alisema kuwa, hatua za Wanadiaspora hao za kutoa huduma za afya kwa jamii ni za kupongezwa na kuungwa mkono na kuadi kutoa mashirikiano makubwa ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa ipasavyo.

Alisema kuwa, zoezi hilo limeweza kuwasaidia wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kusini Unguja pamoja na maeneo mengine ya nje ya wilaya hiyo kutokana na huduma bora zilizotolewa na madaktari hao.

Aliongeza kuwa, wananchi walio wengi wamevutiwa na huduma hizo na wameweza kujitokeza kwa wingi. Sambamba na hayo Mkuu huyo wa Wilaya ya Kusini Unguja alizipongeza juhudi za Serikai ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi za kuendelea kusihirikiana na Wanadisaspora kwa kuisaidia jamii katika kutoka huduma mbalimbali Unguja na Pemba.

Nao wananchi waliofika kupata huduma hizo walitoa pongezi na shukurani zao kwa Madaktari hao waliotoa huduma hizo kwa muda wa siku sita katika hospitali hiyo.

Pamoja na hayo, nao Wanadispora hao waliahidi kuendelea kutoa huduma hizo katika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Huhuma mbali mbali za afya zilitolewa zikiwemo maradhi ya sukari, presha,ngozi, magonjwa ya akina mama, ini, figo, macho na nyenginezo pamoja na kutolewa dawa na miwani kwa wale waliokuwa na matatizo ya macho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news