Mayele rasmi ndani ya Pyramid FC

CAIRO-Klabu ya Pyramid FC ya nchini Misri imetangaza kumsajili mshambuliaji wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Fiston Kalala Mayele (29) kutokea Klabu ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mshambuliaji huyo aneondoka Yanga SC baada ya kucheza misimu miwili Tanzania kwa mafanikio makubwa ambapo msimu wa kwanza 2021/2022 alimaliza nafasi ya pili kwa ufungaji magoli 16.

Aidha, msimu wa 2022/2023 aliibuka MVP wa Ligi Kuu Tanzania Bara sambamba na Tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi sawa na Saido Ntibazonkiza wa Simba wote wakifunga magoli 17.

Nyota huyo ameondoka Yanga SC baada ya kuisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu mara mbili, FA Cup mbili, Ngao ya Jamii mara mbili na kuisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Ni kupitia ushiriki wake ambao kwa mara ya kwanza katika msimu 2022/2023 Yanga SC iliandika historia kubwa ndani na nje ya Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news