Mkwakwani wapewa dhamana ya kufanikisha Ngao ya Jamii

NA DIRAMAKINI

SHINDANO la Ngao ya Jamii ambalo linategemea kuhusisha timu nne ambazo ni Yanga SC, Simba SC, Azam na Singida Fountain Gate FC litafanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Wallace Karia,“Kwenye Ngao ya Jamii ambayo msimu huu zitachezwa mechi tatu.

"Mbili za nusu fainali na moja ya fainali, mechi zote zitachezwa Mkwakwani Tanga kwa sababu Uwanja wa Uhuru na Benjamin Mkapa vimefungwa na Uwanja wa Mkwakwani upo karibu na katika utaratibu mzuri."

Agosti 2022 Bodi ya Ligi (TPLB) ilibadili utaratibu wa shindano la Ngao ya Jamii kutoka mfumo wa timu mbili na kuwa timu nne mwanzoni mwa msimu.

Mfumo wa awali ulikuwa ni mchezo mmoja tu kama unavyofanyika nchi nyingi duniani ukijulikana kwa majina tofauti, lakini kuanzia msimu huu wa 2023/24, Ngao ya Jamii itawaniwa na timu hizo.

“Kutakuwa na shindano maalum la ufunguzi wa Ligi (Ngao ya Jamii) litakaloshirikisha timu zilizoshika nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa Ligi na Timu Bingwa wa Kombe la Shirikisho.

“Endapo bingwa atakua miongoni mwa washindi wa nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, timu iliyoshika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi, itashiriki shindano hilo,” ilielezea sehemu ya taarifa ya bodi hiyo awali.

Kuanzishwa kwa michuano hiyo ya kuwania Ngao ya Jamii, Tanzania itakua na michuano aina tano inayotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuanzia msimu mpya wa 2023/24.

Michuano hiyo ni Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC PL), Ligi Daraja la Kwanza (Championship), Ligi Daraja la Pili (First League), Kombe la Shirikisho (ASFC), Mabingwa wa Mikoa (RCL) na Ngao ya Jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news