Nyumba ya Wazanaki yanogesha Maonesho ya Sabasaba

NA SIXMUD J.BAGASHE

NYUMBA ya asili ya kabila la Wazanaki iliyojengwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taasisi yake ya Makumbusho ya Taifa, imekuwa kivutio kikubwa kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba. 
Makundi makubwa ya wanaofika katika maonesho hayo ya Kimataifa licha ya kupata huduma zingine kwenye Banda la Maliasili na Utalii, wametembelea nyumba hiyo na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu Kabila la Wazanaki lenye historia kubwa kupitia Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mhifadhi mila mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa, Bi. Flora Vincent amesema kuwa, sababu ya kuwa na Onesho la Nyumba ya asili kwenye maonesho hayo makubwa ni kuipa fursa jamii kujifunza umuhimu wa kurithisha kizazi kilichopo mila na desturi za makabila mbalimbali ili kuimarisha Mshikamano wa Kitaifa, Umoja, Upendo, amani kwa maendeleo endelevu nchini.

Akizungumzia maonesho hayo,Debora Danishashe amesema, ameamua kuwaleta wajukuu zake kwenye nyumba hiyo ili wapate uelewa juu ya urithi wa utamaduni, wa makabila mbalimbali ya Tanzania.
Bibi Danishashe ameongeza kuwa, kizazi cha leo kimetawaliwa na ulimwengu wa utandawazi unawafanya waige tamaduni za nje na kusahau zao hivyo ubunifu uliofanywa na Wizara ya Maliasili ya kuwarithisha watu hasa watoto utamaduni wa Kitanzania ni jambo jema la lakupongezwa sana.

Katika nyumba hiyo ya asili ya Wazanaki watu wamepata fursa ya kujifunza kucheza bao, kukumbushwa maadili, aina za vya kula,mavazi ya asili na jinsi ya kuhifadhi mazao kiasili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news