Dkt.Msonde awataka walimu kuwapatia watoto malezi bora na ujuzi

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI 

NAIBU Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Dkt. Charles Msonde amewataka walimu wa elimu ya awali kuhakikisha wanawapatia watoto malezi bora na ujuzi ili wakianza darasa la kwanza wawe na msingi mzuri wa elimu.
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akitoa maelekezo mara baada ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu katika Shule ya Sekondari Mwanzi iliyopo wilayani manyoni. 

Dkt. Msonde ametoa wito huo kwa walimu wote shule za awali nchini, wakati akifungua mafunzo ya walimu 105, Maafisa Elimu Kata 21 na Walimu Wakuu 21 wa Mkoa wa Singida ambayo yatakayowawezesha kutoa elimu yenye tija kwa watoto.

Dkt. Msonde amesema, Serikali inathamini elimu ya awali na ndio maana kupitia mradi wa BOOST madarasa ya awali 12,000 yatajengwa ili kuwezesha shule zote za msingi nchini kuwa na madarasa ya awali kwani miongoni mwa shule zote takribani 17,000 zilizopo baadhi yake tayari zina madarasa ya awali. Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde akizungumza na Walimu, Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wa Mkoa wa Singida wakati akifungua mafunzo yanayolenga kuwawezesha kutoa elimu yenye tija kwa watoto.

“Elimu ya awali inajenga msingi bora wa malezi ya mtoto, tabia nzuri, pamoja na utamaduni wa mtoto kupenda shule, na ndio maana Mhe. Rais aliridhia mradi wa BOOST utengewe trilioni 1.15 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu katika kipindi cha miaka 5 cha utekelezaji wa mradi huo,” Dkt. Msonde amefafanua. 

Ameongeza kuwa, mradi huo umetoa fursa kwa walimu hao kujengewa uwezo wa kutoa mafunzo kwa watoto kwa kulingana na hatua za makuzi.
Kiongozi wa Wawezeshaji, Dkt. Fortunata Pembe akieleza faida ya mafunzo kwa Walimu, Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wa Mkoa wa Singida kabla ya Dkt. Msonde kufungua mafunzo ya watendaji hao yanayolenga kuwawezesha kutoa elimu yenye tija kwa watoto.

Kwa upande wake, kiongozi wa wawezeshaji, Dkt. Fortunata Pembe amesema, pindi walimu hao wakihitimu mafunzo hayo watakuwa tayari kutoa mafunzo kwa walimu wengine.

Naye, Mwalimu Kitila Mkumbo ambaye ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo, ameshukuru kwa kupatiwa mafunzo na kuahidi kuyatumia vizuri ili watoto wapate malezi bora na ujuzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news