Rais Dkt.Mwinyi: Elimu ni kipaumbele cha Serikali

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, sekta ya elimu ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

Ameyasema hayo leo Julai 17,2023 alipoweka jiwe la msingi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kampasi ya Pemba eneo la Mtima Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

Pia, Rais Dkt.Mwinyi ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuona umuhimu wa kufungua kampasi hiyo kisiwani Pemba ikiwa ni sehemu sahihi ya kusogeza huduma za jamii katika sekta ya elimu kwa watu wa Pemba na Watanzania kwa ujumla.

Vilevile, Rais Dkt.Mwinyi alieleza kuwa, mchango mkubwa wa chuo hicho kwa taifa na uzoefu waliokuwa nao wa kutoa mafunzo kwa wahitimu walioiva kimaadili, kiuongozi, uadilifu, uzalendo na weledi wa hali ya juu ambazo ni nyezo muhimu kwa mtumishi yoyote anayepewa dhamana ya utumishi wa umma.

Katika hatua nyingine,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewakabidhi kompyuta mpakato wanafunzi wa kidato cha nne na sita waliofanya vizuri kwenye mitihani yao ya taifa ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Ikulu jijini Zanzibar.

Hafla hiyo ya kuwazawadia kompyuta mpakato wanafunzi hao imefanyika leo ukumbi wa Tibirinzi Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali imejikita kwenye kuimarisha miundombinu kwa Skuli zote ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi wengi ikiwemo kuondosha mikondo kwa skuli zote za Unguja na Pemba kwa kuendelea kujenga Skuli za ghorofa za Msingi na Sekondari ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kuhudhuria masomo ya madrasa wakati wa jioni kwa kuwa na mkondo mmoja.

Kwa upande mwingine miongoni mwa wanafunzi waliowakilisha wenzao kupokea kompyuta hizo ni Hajra Khamis Ali, Haitham Omar Abdallah na Salum Ahmed Nassor wote kutoka Skuli ya Sekondari ya Fidel Castro na Lukman Mohamed Ali kutoka Skuli ya Sekondari Chasasa, Wete Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news