Stendi ya Magufuli yamtoa machozi Mwinjilisti Temba

NA DIRAMAKINI

MWINJILISTI wa Kimataifa, Alphonce Temba ameonesha kusikitishwa na hali ilivyo katika Stendi ya Kimataifa ya mabasi ya Magufuli iliyopo Mbezi Luis katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo anasema kwa sasa thamani yake haipo kutokana na wafanyabiashara wa mabasi kuamua kila mmoja kutumia eneo lake.

Kutokana na hali hiyo,ameiomba Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kuchukua hatua madhubuti ambazo zitawezesha heshima ya stendi hiyo kuwepo na thamani yake kuonekana kwa Watanzania wakiwemo wageni kutoka mataifa mbalimbali.

"Kitendo cha kuendelea kutokubanwa kwa wafanyabiashara wa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani kupaki eneo moja la Mbezi katika stendi ya Magufuli kina athari nyingi sana kwa Watanzania na mwananchi mmoja mmoja zisizoonekana na zenye madhara makubwa sana na maumivu makubwa sana kwa Watanzania wenye kipato cha chini.

"Yapo mambo ambayo yanatokana na mfumo huo wa ovyo na mbaya uliokubalika sasa na haukuwa mfumo wa kawaida kwa sababu hata hapo mwanzo haukuwa kwa stahili hiyo wakati mabasi yakipaki Ubungo.

"Pamoja na kwamba tumejenga stendi kubwa na mabasi yote yana uwezo wa kuwa pale, lakini kitendo cha Serikali kuruhusu mabasi yaendelee kukaa kila sehemu mfano kutoka Mbenzi-Magufuli kwenda mpaka Ubungo-Mataa ambako kulikuwa na stendi ya awali si mahali parefu sana ambapo hapazidi kilomita tano.

"Na kumekuwa na mabasi sasa yamewekwa kabisa barabarani kwenye sheli pale Ubungo Plaza hapo Shekilango kwenye Nyumba za Urafiki ambazo hazina miundombinu, hazikutengenezwa maalumu kwa ajili ya kuwa stendi ya mabasi.

"Zimegeuzwa bila kuzingatia mashariti na kanuni za kupaki eneo la parking tunaweza kuona kama Mlimani City ni maduka, wametengeneza eneo maalumu la parking na eneo la ulinzi maeneo haya ambayo yametengenezwa kwa kuweka tu kutumia eneo ambalo halikuwa designed kugeuzwa kuwa eneo.

"Kwanza lilikuwa eneo korofi limeendelea kusababisha ajali na limezuia njia, linanyima watu uhuru hawa wote ni wafanyabiashara ndio wamekuwa na nguvu kuyafanya haya bila kufuata masharti.

"Manzese pale kuna parking ya mabasi kwenda mikoani, Kinondoni parking ya mabasi ya kwenda mikoani na yanapaki service road, yanapaki ovyo yanajaza watu.

"Sasa pale Mbezi ambako ndiko Magufuli Terminal kuna watu ambao ni Watanzania kina mama, wazee wasichana ambao wamefungua biashara zao kule juu wakiwategemea abiria wanunue biashara zile zinakuwa zinadoda.

"Biashara zile zinakosa wateja, wametumia fedha zao na mitaji yao wanasomesha wanafamilia na wana wazazi wanawasaidia kwa sababu ya uholela huu unasababisha wale watu wanakosa riziki kwa sababu ya kupaki hovyo hovyo.

"Matokeo yake pia hawa vijana ambao ni wavivu wanazidi kuongezeka hawataki kulima, hawataki kufanya kazi, badala yake wanabaki pale stendi eti wanawaelekeza watu stendi inaingia wapi akilini hata nchi zinazotunguka sisi Kenya, Uganda, Rwanda Zambia, Malawi, Msumbiji hakuna wapiga debe wanaojazana zaidi watu zaidi ya 1,000 wako stendi wanawaelekeza watu kupanda mabasi.Wale kwa asilimia kubwa ni wezi.

"Wako pale kwa lengo la kuwaibia watu hicho kitu hakipo, mabasi yanajulikana, mabasi yana makondakta, madereva, na madereva wa ziada wanashindwaje kufanya hiyo kazi?.

"Kule ndani kwa Magufuli pako vizuri kabisa, basi linakwenda mkoa gani, kondakta yuko pale kabisa akipokea watu na kuwakatia risti leo wapo vijana wanaoranda randa eti wapiga debe wamejazana na sijui hata kama wanalipa fedha za kuingia mle ndani.

"Hao watu wanakuja kuwa bomu la baadae kwa sababu wanatengenezewa mazingira yasiyofaa wanakuwa wavivu wa kufanya kazi na shughuli za uzalishaji matokeo yake basi likishatoka pale saa mbili watu wanakuwa wa kubahatisha kuingia mle ndani, matokeo yake kule nje kuanzia Morogoro-Road na barabara nyinginezo zilizoko karibu na Magufuli wako vijana kazi yao kuwatoa watu kule Magufuli kuwapeleka kwa Yusuph pale ambako kuna watu wanasimamisha magari ya private, hivyo kuna mtandao kabisa wa baadhi ya watu wanaokwenda mikoani hasa Dodoma, Mbeya, Arusha, Mwanza, Singida wanapigiana simu wanawashawishi watu kuwa kuna Prado, kuna Costa na kuna gari fulani inayoenda kwa haraka gharama yake nafuu toka twende.

"Matokeo yake stendi ya Magufuli imekuwa haina thamani na ni stendi bora ina mwelekeo kama Airport hakuna stendi yoyote Afrika iliyojengwa yenye mandhari yenye ubora kama hii, hii stendi bora Afrika nzima lakini mpangilio uliowekwa ni mbovu.

"Matokeo yake ndio hayo uholela hata hapo Nairobi hakuna vijana wa kupiga kelele na kusema eti wanamtoa mtu stendi au wanampeleka mtu stendi kwa kumnyang'anya begi kama kibaka.

"Hawa vijana wanaokwenda pale kwa asilimia 70 hadi 80 ni wavivu hawataki kufanya kazi wanapata fedha na bahati mbaya hata fedha wanazozipata kwa kuwa kesho wanajua watazipata wanaishia kwenye umalaya, uzinzi na kueneza hata HIV kama Serikali haitafanya juhudi kuwaondoa hao vijana ili stendi yetu iwe kama Airport.

"Kwa nini Mwalimu Nyerere International Airport hakuna vijana wanaosimama pale kupeleka watu kwenye ndege kwa nini?,

"Kwa sasa nchi ipo kwenye mfumo wa kidigitali kwa maana kutakuwa na ununuzi wa tiketi kwenye mtandao ukienda kwenye stendi unaenda kwa appointment, hawa vijana wataendelea kuchelewesha.

"Kwa hiyo, naiomba serikali namuomba Waziri Mkuu magari yote yarudi pale kwenye Stendi ya Maguli tulitendee heshima hata jina la kiongozi wetu aliyetutoka na stendi hiyo hadhi yake iko juu wanakuja wageni kutoka nje wanakiri hawajawahi kuona stendi nzuri na bora kama stendi ya Magufuli, lakini tunavyoichukulia sisi Watanzania kwa kweli tunaiweka kwenye kiwango cha chini sana na hawa vijana wanaoranda randa kunyang'anya watu mabegi wako mpaka kwenye stendi ya daladala mtu anaposhuka kwenye stendi ya daladala imekuwa ni kero mtu anashambuliwa kama jambazi wanakuharasi.

"Mtu unataka utaratibu na ustaarabu kumbuka kuna watu wanasafiri kwenda kwenye mambo yao ya maana, lakini wanasumbuliwa sana.

"Hiyo ndio shida vijana wengi wanakuwa wapiga debe na wavivu, huu mfumo hauko nchi nyingine uko Tanzania peke yake wa kuzalisha vijana wapiga debe na wanapata fedha wanazitumia kunywa na kufanya starehe wanajua kesho watapata, kesho kutwa watapata naomba Serikali iangalie huu mfumo kama unafaa urasimishwe,"amefafanua Mwinjilisti Temba Juni 30, 2023 wakiti akizungumzia kuhusiana na namna ambavyo wafanyabiashara wa mabasi wanaendelea kushusha thamani ya stendi hiyo jijini Dar es Salaam

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news