Tutaendelea kuelimisha umma masuala ya maafa-Dkt.Yonazi

NA MWANDISHI WETU

OFISI ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge kupitia Idara ya Menejimenti ya Maaafa imesema, itaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na majanga mbalimbali pindi yanapotokea ili kupunguza athari za majanga hayo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Mkurugenzi Msaidi Utafiti Idara ya Menejimenti ya Maafa, Bw.Charles Msangi (wa kwanza kushoto) alipotembela banda la ofisi yake katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba leo Julai 6, 2023 jijini Dar es Salaam.(Picha na OWM).

Akizungumza leo Julai 6, 2023 wakati alipotembelea Maonesho ya Kimataifa ya 47 ya Biashara maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Dkt.Jim Yonazi amesema kuwa, Serikali inaendelea kushirikiana na wadau ili kuhakikisha kuwa uwezo wa nchi katika kukabiliana na majanga mbalimbali pindi yanapotokea unaboreshwa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt.Jim Yonazi akiangalia moja ya kitabu wakati alipotembelea katika banda la Idara ya Menejimenti ya Maafa lililo chini ya ofisi yake katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Ameongezea kuwa, Serikali itaendelea kuratibu vyema masuala ya menejimenti ya maafa kwa kuzingatia mifumo ya kitehama ili kuwafikia wananchi kwa wakati kuendelea kuleta matokeo yanayokusudiwa. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt.Jim Yonazi akiangalia moja ya kitambulisho cha waandishi wa habari (press card) wakati wa ziara yake banda la Idara ya Habari Maelezo, kulia ni Afisa habari Idara ya Habari Maelezo, Bi.Lilian Lundo.
Afisa Masoko kutoka TSN, Bi.Anitha Shayo akimkabidhi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt.Jim Yonazi nakala ya magazeti yanayochapiswa na taasisi hiyo alipotembelea katika banda lao katika maonesho ya Kimataifa ya biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

“Serikali imewekeza katika mifumo mbalimbali ya kiteknolojia inayosaidia kutoa viashiria vya awali vya majanga na pia kusaidia katika utoaji wa taarifa kwa haraka,”ameeleza Dkt.Yonazi.
Afisa TEHAMA Kutoka TSN, Bw. Prosper Mallya akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi namna mifumo ilivyoboreshwa na taasisi hiyo alipotembelea banda la TSN katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) jijini Dar es Salaam Julai 6, 2023.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza jambo kuhusu uboreshwaji wa mifumo ya TEHAMA na Afisa TEHAMA wa taasisi hiyo, Bw. Prosper alipotembelea banda la lao Julai 6, 2023 Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Pia akieleza mikakati ya Serikali kuratibu masuala ya maafa alisema, imejipanga kuufikia umma wa Watanzania kuanzai ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa hadi Taifa na kwa kuzijengea uwezo kamati za maafa kwa ngazi zote na kuwa na jamii stahimilivu ya maafa nchini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi (mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi yake alipotembelea banda la Idara ya Menejimenti ya Maafa katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

“Katika mwaka huu mpya wa fedha, tumejipanga kuendelea kujenga uwezo kwa wadau wetu ili kuhakikisha uwezo wetu wa kukabiliana na majanga aina mbalimbali unaboreshwa kwa kuzingatia athari zake kiuchumi, kijamii na nyingine nyingi,”amesisitiza Dkt.Yonazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news