VIDEO:Mwinjilisti Temba afichua stendi kituo cha mafuta

DAR ES SALAAM-Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba amefichua uwepo wa stendi mbadala ya mabasi yaendayo mikoani katika kituo cha mafuta kilichopo mkabala na Ubungo Plaza ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Uwepo wa kituo hicho ambacho si rasmi, Mwinjilisti Temba anasema licha ya kudhoofisha Stendi ya Kimataifa ya Magufuli iliyopo Mbezi jijini humo pia kinahatarisha usalama wa abiria wanaosafiri kwenda mikoani.

"Haya ndiyo mazingira ya Ubungo Plaza katika Sheli ya Engen, ndiyo pamegeuka stendi ya mabasi yaendayo mikoani, hawa ni abiria wamekaa barabarani wakisubiri  mabasi kwenda mkoani.

"Stendi ya Magufuli, ni stendi ambayo ni bora zaidi Afrika na imewekwa makusudi kwa ajili ya kuhudumia mabasi yote, lakini hawa matajiri wenye fedha na wafanyabiashara wanaoiyumbisha Serikali ndiyo wameamua kuweka stendi za mabasi popote wanapotaka.

"Wameamua kuweka stendi za mabasi hapa ni barabarani kabisa na ukiangalia hii ni services road na ikumbukwe kwamba kilomita moja ya lami ni zaidi ya bilioni moja, sasa hapa ndiko watu wanasubiria mabasi ya kwenda mikoani katika sheli ni hatari, mtu akivuta sigara, sheli ikilipuka ndipo hapo sasa watu wataambiwa waende Magufuli kule.

"Niiombe Serikali, nimuombe Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kweli hii haikubaliki, hii haileti afya, hawa wafanyabiashara na wengine ni wabunge ndio wanaoisumbia nchi hii, na ndio wanaolivuruga hili Taifa na siyo wapinzani, ni hawa hawa ambao wengi wetu ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, lakini ni wafanyabiashara ndiyo wenye magari na ndiyo wabunge hawa.

"Ambao wanatunga sheria, hapa ni Engen opposite na Ubungo Plaza, lakini pamekuwa stedi ya mabasi unaona abiria wamekaa chini pale, hivi gari limekosea...likamgonga mtu pale ndipo hapo watu wataambiwa waondokle, yaani watu wamekaa barabarani kabisa, kama unavyoona magari yanapita hivi ndivyo yanavyopakia mabasi ya kwenda mikoani ya kwenda Morogoro, ya kwenda Dodoma, ya kwenda Singida kwenda mikoani.

"Mimi ninadhani Serikali iliangialie sana jambo hili, jambo hili ni aibu na haliwezekani kabisa kwa nchi yetu yenye utaratibu mzuri, watu wanakaa na familia zao na wana mizigo yao, wengine wanaingia na kushushwa barabarani mimi ninadhani hiki kitu haikubaliki kabisa,"amefafanua Mwinjilisti Temba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news