Watembelea miradi ya maendeleo Kata ya Nyasho

NA FRESHA KINASA

KAMATI ya Siasa ya Kata ya Nyasho katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara imefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika kata hiyo kwa kipindi cha Januari hadi mwezi Juni 2023 ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2020.
Kamati hiyo imefanya ziara hiyo hivi karibuni ambapo miradi mbalimbali iliyotembelewa ni iliyotekelezwa katika kipindi hicho ni miradi ya ujenzi wa Karavati tatu, ujenzi wa mitaro mita 450, kutembelea vikundi vya akina mama na vijana vilivyopewa mikopo kwa nyakati tofauti.
Pia, kamati hiyo ya siasa ilitembelea mradi wa ukarabati wa Shule ya Msingi Nyasho 'B' ambayo ilitengewa fedha kiasi cha shilingi millioni 90 kwa uboreshaji wa majengo.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Nyasho, Jumapili Mboga akipokea taarifa, amempomgeza Diwani wa Kata ya Nyasho, Mheshimiwa Haji Mtete kwa namna ya kipekee anavyoendelea kusimamia ilani hiyo na namna anavyotekeleza maagizo ya chama katika kuhakikisha miradi inawanufaisha wananchi.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo, Mheshimiwa Haji Mtete amesema atahakikisha kata hiyo inaendelea kupata maendeleo kwa kuwatumikia wananchi kwa dhati.

Pia, amemuomba mkandarasi aliyechukua tenda ya ukarabati wa Shule ya Nyasho ambalo ni Jeshi la Magereza kukamilisha ujenzi huo kwa haraka ili wanafunzi wanapofungua wasome kwa ufanisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news