Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje waonesha vipaji dimbani

NA MWANDISHI WETU 

WATUMISHI wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo Julai 7, 2023 kwa shauku na morali ya hali juu wameshiriki bonanza la michezo lililofanyika kwenye uwanja wa Dodoma Sekondari jijini Dodoma.
Timu ya mpira ya miguu ikiongozwa na nahodha wake Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi wakiwa kwenye picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuwakabili wapinzania wao kwenye bonanza la michezo lililofanyika katika uwanja wa Dodoma Sekondari jijini Dodoma.

Bonanza hilo ambalo limeandaliwa na Wizara limehusisha michezo mbalimbali kama vile mazoezi ya pamoja ya viungo, mpira wa miguu, mpira wa pete na riadha.

Bonanza hilo pamoja na masuala mengine lililenga kuhamasisha upimaji wa afya kwa watumishi wake hususani kwa Magonjwa Sugu Yasiyoabukiza (MSY), ikiwa ni miongoni mwa hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na wizara katika utekelezaji wa Afua za VVU na MSY kwa mujibu wa Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza wa mwaka 2014. 
Washiriki wa michezo wakiwa katika hali ya furaha kwenye ufunguzi wa Bonanza la michezo lililofanyika katika uwanja wa Dodoma Sekondari jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Chiku Kiguhe ameeleza kuridhishwa kwake na namna watumishi walivyohamasika kushiriki zoezi la upimaji afya na michezo ya pamoja. 
Wachezaji wa mpira wa pete wakiwania mpira kwenye bonanza la michezo lililofanyika katika uwanja wa Dodoma Sekondari jijini Dodoma.

Vilevile, ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa Watumishi wa Wizara kuendelea kujitokeza kwa wingi katika kushiriki michezo, kupima afya mara kwa mara na kuzingatia ushauri na miongozo inayotolewa na wataalam wa afya kuhusu masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha afya zao. 
Wachezaji wa mpira wa miguu wakiwania mpira kwenye bonanza la michezo lililofanyika katika uwanja wa Dodoma Sekondari jijini Dodoma.

Watumishi wa Wizara waliojitokeza katika bonanza hilo kwa nyakati tofauti wameeleza furaha yao kuhusu namna Uongozi wa Wizara unavyozigatia na kujali suala la utimamu wa afya ya Watumishi wake, hususani kwa kuandaa programu mbalimbali za mara kwa mara ikiwemo michezo, elimu kuhusu masuala ya afya na upimaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news