Waziri Dkt.Mabula asisitiza manufaa ya Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi nchini

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ametaka wananchi wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha kutumia fursa ya Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi nchini kutatua migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu katika halmashauri hiyo.

Dkt.Mabula ametoa kauli hiyo leo Jula 8i 2023 wilayani Longido mkoa wa Arusha wakati akifungua Mkutano wa wadau kujadili Mpango wa Matumzi ya Ardhi wilaya ya longido uliobeba kauli mbiu ya uboreshaji milki kwa maendeleo endelevu.

Amesema, halmashauri ya wilaya ya Longido inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo muingiliano wa aina za ardhi. Kwa mujibu wa Dkt Mabula changamoto hizo zimesababishwa na taasisi mbalimbali kufanya kazi katika eneo moja kwa nyakati tofauti pasipo kushirikiana.

‘’Pamoja na changamoto hizi serikali imelazimika kuichagua Halmashauri ya Wilaya ya Longido kuwa miongoni mwa halmashauri saba zinazotekeleza shughuli za urasimishaji ardhi ya vijiji kupitia mradi wa kuboresha usalama wa milki."

Amewataka washiriki wa mkutano huo kutumia Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi kama fursa na kuwataka viongozi na wananchi wa Wilaya ya Longido kutoa ushirikiano thabiti ili kufanikisha utekelezaji wake.
‘’Maeneo mengi yalitamani kupata fursa kama hii lakini kutokana na uchache wa rasilimali hawakufanikiwa kufikiwa na mradi, nashauri tumieni fursa hii kikamilifu kwa maendeleo ya wilaya na mkoa wa arusha kwa ujumla.’’

Aliongeza kuwa, katika kuongeza juhudi za serikali kutatua changamoto zinazoikabili halmashauri ya wilaya ya longido, Wizara ya Ardhi imewezesha halmashauri hiyo kuandaa Mpango wa Matumizi ya Ardhi wenye mapendekezo ya maeneo yaliyopaswa kubaki kuwa ardhi ya vijiji ikiwa ni pamoja na ardhi kwa ajili malisho, ardhi ya hifadhi na maeneo ya ardhi ya jumla.

Kwa mujibu wa Dkt.Mabula, mapendekezo hayo yamewasilishwa katika mkutano huo kujadiliwa kwa pamoja na kufanya maboreshio stahili ili mpango huo uwe unatambulika na kukubalika na wadau wote.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marco Ngumbi amewataka washiriki wa mkutano huo kuwa, makini wakati wa utekelezaji Mpango wa Matumizi ya Ardhi katika halmashauri ya Longido huku akitaka kuheshimiwa kwa wataalamu pale linapofanyika suala la kitaalam. Alitoa tahadhari kwa viongozi wa halmashauri hiyo na kauli wanazotoa wakati wa utekelezaji wa mradi.

‘’Ni muhimu kwa viongozi kuwa na tahadhari ya kauli, maneno na mienendo pale linapotokea suala la utalaamu na kinachofanyika sasa katika mradi siyo kipya kilifanyika katika serikali za awamu zote kuanzia ya kwanza hadi ya sasa.’’
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Wadau kujadili Rasimu ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya wilaya ya Longido leo Julai 8,2023. (Picha na Wizra ya Ardhi).

‘’Pamoja na changamoto hizi serikali imelazimika kuichagua halmashauri ya wilaya ya Longido kuwa miongoni mwa halmashauri saba zinazotekeleza shughuli za urasimishaji ardhi ya vijiji kupitia mradi wa kuboresha usalama wa milki."

Meneja Urasimishaji Ardhi ya Vijiji kupitia Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi, Joseph John Osena amesema, mkutano huo wa Wadau kujadili Mpango wa Matumizi ya Ardhi unatoa fursa kwa wadau kujadiliana kuhusu mpango sambamba na kuwa na usalama wa maeneo yao.

‘’Kupitia mradi wa uboreshaji usalama wa milki hati zinaenda kutolewa katika vijiji na srerikali inataka kuona wananchi wake wako salama na Longido ni moja ya wilaya chache zinazofikiwa na mradi."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news