Waziri Mkuu amtaka Balozi Bakari akadumishe Diplomasia ya Uchumi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki, Seif Idd Bakari aweke msisitizo katika kusimamia utekelezaji wa sera ya mambo ya nje ikiwa ni pamoja na kudumisha diplomasia ya uchumi, kuhamasisha uwekezaji na upatikanaji wa masoko wa bidhaa za ndani.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki, Seif Idd Bakari Ofisi kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam leo Julai 5, 2023 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

“Kupitia mahusiano haya, zipo fursa nyingi ambazo tunahitaji kuzipata hasa za kiuchumi, Tanzania ni nchi ambayo inazalisha na inauza tukiwa peke yetu hatuwezi kumudu ndio maana tunashirikiana na mataifa mbalimbali kupitia mabalozi wetu”

Waziri Mkuu amesema hayo leo Julai 5, 2023 alipokutana na Balozi huyo ofisini kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Majaliwa pia amemtaka Balozi Seif aweke mikakati itayoiwezesha nchi kunufaika na uwepo wake ikiwemo kusimamia mahusiano ya kibiashara “Tunakaribisha wafanyabiashara kwenye nchi yetu, tunahitaji kupata wawekezaji, wakija nchini tutanufaika kwa kupata teknolojia mpya na kuongeza idadi ya ajira kupitia uwekezaji wao”

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Balozi Seif atumie fursa hiyo kuitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuongeza idadi ya watalii wanaoitembelea Tanzania. “Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alianzisha program ya Royal Tour ambayo imevutia nchi nyingi, nenda kapime kwenye nchi yako wangapi wanaifahamu Tanzania, katumie majukwaa mbalimbali ya kuitangaza nchi yetu”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Balozi Seif kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa mbalimbali zinazotoka nchini “Uzalishaji wetu ni mkubwa na msisitizo bado unaendelea kupitia Sera ya nchi na Jumuiya zetu ikiwemo EAC na SADC tumekuwa na mkakati wa uzalishaji ili tuweze kuuza na kupata Dola.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news