Waziri Mkuu wa Japan ziarani Saudi Arabia

TOKYO-Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa Fumio Kishida ataanza ziara nchini Saudi Arabia leo Jumapili ya Julai 16,2023.

Hayo ni kwa mujibu wa Nikkei ambalo limeripoti kuwa, Mheshimiwa Kishida akiwa nchini humo anatarajiwa kukutana na Mwanamfalme Mohammad Bin Salman. Pia, nchi hizo mbili zinatarajiwa kukubaliana kuhusu uwekezaji wa pamoja ili kuendeleza rasilimali adimu duniani.

Kwa mujibu wa tarifa za Nikkei, Mheshimiwa Kishida anazuru Saudi Arabia kama sehemu ya ziara ya Mashariki ya Kati.

Aidha, kupitia makubaliano hayo, mkataba wa ushirikiano utatiwa saini hivi karibuni na Wizara ya Uchumi, Biashara na Viwanda ya Japan, Shirika la Usalama wa Metali na Nishati la Japan (JOGMEC) linaloungwa mkono na Serikali na Wizara ya Viwanda na Rasilimali za Madini ya Saudi Arabia.

Chini ya mpango huo, Japan na Saudi Arabia zitachunguza miradi ya maendeleo ya rasilimali katika nchi za tatu kwa uwekezaji wa pamoja. Vilevile, mataifa hayo kwa pamoja yanatarajia kupata haki za madini muhimu, kama vile metali adimu zinazotumika katika magari ya umeme.

Mahitaji ya EVs yanaongezeka tu huku kukiwa na msukumo wa kimataifa kuelekea uondoaji kaboni. Mheshimiwa Kishida pia anatarajiwa kufika Umoja wa Falme za Kiarabu na Qatar kukutana na viongozi wao huku wakitarajiwa kuthibitisha ushirikiano katika nishati na nyanja nyinginezo. (Nikei/SG/DIRAMAKINI)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news