Fahamu kwa nini kampuni mbili tanzu ndani ya TPDC

NA GODFREY NNKO

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame amesema, sababu moja wapo iliyochangia kuanzishwa kwa kampuni tanzu ndani ya shirika hilo ni ili kuongeza ufanisi na kuleta matokeo bora.
"Tumekutana hapa kwa dhumuni la kushiriki hafla ya uzinduzi wa bodi za kampuni tanzu za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)."

"Napenda kutoa shukurani kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika hafla hii, pia kukubali na kuendelea kuendeleza dhamira ya dhati ya Serikali kuliwezesha shirika liwezeshe uwezo wa ufanisi wa hatua za uendeshaji wake kibiashara na ushindani ndani na nje ya nchi, kikanda na kimataifa."

"Pia nashukuru kwa uwepo wa Ofisi ya Msajili wa Hazina kupitia wawakilishi wao, napenda kuwapongeza wajumbe wa kampuni tanzu ambao wameteuliwa na leo bodi zao zitakuwa zinazinduliwa japokuwa wameshaanza kazi.

"Tutakuwa wakosefu wa fadhila tusipotoa shukurani zetu kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madatakani mwaka 2021 tukaona jitihada zake za dhati na makusudi za kuweka kipaumbele katika sekta ya nishati.

"Hususani katika shirika letu la TPDC pamoja na mambo mengine dhamira hiyo imeoneshwa na Serikali kuendelea kuwekeza katika miradi mikubwa ikiwemo bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki.

"Mradi wa uchakataji na usindikaji wa gesi asilia na LNG kule Lindi pamoja na miradi yetu mingine ikiwemo ya utafutaji wa mafuta na gesi na miradi mingine ya usambazaji wa gesi."
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC ameyabainisha hayo leo Agosti 31, 2023 katika hafla ya uzinduzi wa bodi za kampuni tanzu mbili za Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) ikiwemo Kampuni ya Gesi Tanzania (GASCO) na Kampuni ya Mafuta (TANOIL).

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Balozi Ombeni Sefue.

"Katika kuyatekeleza haya, tunafahamu toka mwaka 1969 TPDC ilipoanzishwa na kuanza shughuli zake mwaka 1973 kumekuwa na mafanikio makubwa.

"Lakini ilionekana kwamba, baadhi ya majukumu ya shirika ili yaweze kutekelezwa kwa ufanisi, shirika liwe na kampuni tanzu. 

"Hivyo mwaka 1985 GASCO iliundwa, lakini kwa sababu mbalimbali haikuweza kuanza utekelezaji wa shughuli zake. 

"Mwaka 2014 wakati tunaelekea kuzindua mradi wa bomba la gesi na mtambo wa uchakataji wa gesi asilia Songosongo na Madiba ikaonekana sasa ni wakati wa GASCO kuanza kazi zake na hivyo GASCO ikafufuliwa na kuwekwa sawa na wafanyakazi kuanza kuajiriwa.

"Mpaka sasa GASCO ina wafanyakazi zaidi ya 200 katika maeneo ya Kinyerezi hapa Dar es Salaam, Kilwa, Songosongo na Madiba kule Mtwara.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji huyo alifafanua kuwa, "Tarehe 22 Machi 1999, shirika pia lilianzisha kampuni ya mafuta wakati huo ikiitwa Commercial Petroleum Company.

"Lakini nayo kwa sababu mbalimbali haikuweza kuanza shughuli zake rasmi mpaka ilipofika mwaka 2017 ikianzishwa na kisha kubadilishwa jina ikawa TANOIL Investment kwa sasa hivi ina wafanyakazi zaidi ya 20.

"Tangu kuanza kwa Kampuni ya TANOIL na GASCO utekelezaji wa majukumu yake ulisimamiwa na bodi za mpito ambazo kwa kiasi kikubwa ziliundwa na Bodi ya Wakurugenzi TPDC.

"Bodi hiyo ilimaliza muda wake mwaka 2019 mwezi Mei na kwa kipindi cha takribani miaka mitatu bodi ya TPDC kwa vile haikuwepo na hizi kampuni tanzu ambazo hazina bodi majukumu ya bodi ya TPDC yalikuwa yakiendelea kusimamiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati.

"Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati aliendelea na jukumu hilo mpaka mwezi Mei 2022 pale Mheshimiwa Rais alipokuteua kuwa Mwenyekiti na Waziri wa Nishati alipoteua wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi tarehe 10 Juni 2023 na kuizindua bodi hiyo mwanzoni mwa mwezi Julai 2023."
"Mheshimiwa mgeni rasmi, utakumbuka bodi yako ilitoa maelekezo kwa menejimenti ya TPDC kuanzisha mchakato wa kuwapata wajumbe wa kampuni tanzu, na leo tunapenda kuufahamisha umma kwamba zoezi hili lilikamilika kutekelezwa kwa misingi ya uwazi na weledi mkubwa na leo tupo katika hafla ya uzinduzi wa bodi hizo."

"Mheshimiwa mgeni rasmi, TPDC kama kampuni mama tunafarijika kwa kupatikana kwa bodi hizi za kampuni tanzu hasa baada ya kukaa kwa kipindi kirefu bila kuwepo kwa bodi zenyewe."

"Naungana na Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC na menejimenti za shirika na kampuni tanzu kuwapongeza wajumbe wateule wa bodi hizo kwa kujitoa ili kutumikia kampuni tanzu."

"Pia, napenda kuwahimiza kutelekeza majukumu yao kwa weledi na uzalendo ili kutetea masilahi ya taifa letu na kutimiza adhima ya kurejesha shirika na hizi kampuni kibiashara."

"Niwashukuru Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wizara ya Nishati na Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC kwa ushirikiano mkubwa ambao wametuonesha katika ustawi wa shirika na ushirikiano huo ni kuonesha kwamba tunaweza kujiendesha kibiashara na kutimiza malengo ya shirika."

Mwenyekiti wa Bodi ya TAOIL na GASCO

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi za kampuni hizo mbili,William Chiume amesisitiza kuwa, maelekezo ambayo yametolewa na viongozi hao watayafanyia kazi kwa ukamilifu ili kupata matokeo bora.
"Maelekezo yaliyotolewa tutayafanyia kazi vizuri, kitu muhimu ni kwamba tunaendeleza dhamira ya TPDC ya kujiendesha kibiashara na pia adhima ya serikali.

"Na kuhakikisha usalama wa kutosha upande wa nishati na mafuta. Ningependa kusema kwamba katika shughuli zetu tutahakikisha kila mtu anarudi nyumbani salama na wale ambao tunaofanya nao kazi na wale ambao tunawagusa katika shughuli zetu.

"Kwa hiyo, pia tutahakikisha usalama wa mazingira,kuboresha mazingira na miundombinu."Kama mnavyofahamu miundombinu ya nishati ya gesi ni muhimu sana kwa sababu na GASCO wana-provide nishati ya gesi katika kuendesha nishati ya umeme wamefikia asilimia 60 mpaka 70 kwa hiyo ni muhimu sana.

"Kwa ufupi jukumu mlilotupa ni kubwa na tunalifahamu, tunawashukuru sana hata watu mliotuchagulia wana uzoefu, wataboresha hizi kampuni zitakavyofanya kazi na uzuri mimi niko huku na huku.

"Yale mazuri ambayo yatakuwa yanaongelewa upande mmoja, mimi nitayapeleka upande mwingine.
"Kwa hiyo issue ya integrity, professionalism pamoja na respect ni kweli tutaji-organise, tuta-establish structure, mpaka na katika mambo yale ya financial, kufuatilia yale mambo ambayo yako kwenye TPDC bord kutoa ripoti kuweza kujipima utendaji wetu kama kuna matatizo tunayagundua kabla hayajawa makubwa."

"Ku-establish documentation ambazo zitatu-govern sisi wenyewe pale ndani pamoja na mahusiano yetu sisi wenyewe pamoja na manegement ya TPDC na bodi ya TPDC."

"Upande wa GASCO wanafanya na wanaendesha ile mitambo ya kuchakata gesi pamoja na bomba, lakini ingekuwa vyema wangeweza kufanya zaidi."

"Kwa mfano tunapozungumzia katika shughuli za CNG (Compressed Natural Gas) ambayo ni timu muhimu sasa, hapa tunakipaumbele. 

"GASCO vile vile katika shughuli za LNG hata kama haitatokea leo ama kesho, lakini tunaanza kujitayarisha kwenda mbele.

"Tuna mazungumzo na Mozambique ikiwezekana kabda tunaweza tukaunganisha mfumo wao na wa kwetu na data ziko pale Mtwara iko karibu na hii mifumo.

"Kwa hiyo tukiunganisha GASCO karibu na hiyo infrastracture kuhakikisha inatekelezeka pamoja na ambition zetu za ku-establish Petro Chemical Industry pale Lindi karibu na ile saiti.
"Jukumu ambalo tunaweza kulichukua upande wa GASCO wawe mstari wa mbele katika hilo."Upande wa TANOIL Mwenyekiti wa bodi wiki iliyopita tulikutana na wajumbe wa bodi wa TANOIL wakashituka kidogo. 

"Maana kuna changamoto nyingi, lakini tunashukuru mmetupa jukumu hili mmetuamini tuweze kwenda mbele na huko mbele tunaahidi kufanya mengi nafikiri mwakani wakati kama huu tutakuwa vizuri."

"Tutahakikisha madeni yote ambayo TANOIL inawadai wale ambao wametusumbua huko nyuma tunaweza kuyatatua system control, procedures, policy, process governing structure zitakuwa established soon as possible."

"TANOIL vile vile tutakuwa tunajikita katika mambo ya storage ili mambo ya mafuta yasije yakawa matatizo,"amefafanua kwa kina Mwenyekiti wa bodi hizo mbili.

Muhimu

Awali akiwasilisha wasilisho katika hafla hiyo, Dkt.Elias Mwashiuya alifafanua kuwa,mwaka 2015 TPDC ilipata hadhi ya kuwa shirika la taifa la mafuta.

Dhamira ikiwa ni kulifanya liwe na maono makubwa zaidi kama yalivyo mashirika mengine duniani.

"Mpaka leo hii tuna wafanyakazi 499 na kati yao 460 ni wa kudumu na hawa wengine ni kutoka taasisi nyingine ili kwenda katika mradi wa ECOP pia tunazo ajira za muda 26."

"Kampuni tanzu ilianza kitambo kidogo, lakini mwaka 2014 na 2015 tumeweza kutekeleza majukumu yake kama Sheria ya Petroli inavyotaka.
"Ndio maana sasa bodi ya TPDC iliweza kuona umuhimu kampuni tanzu ziwe na bodi zake ku-overcome changamoto na kutoa miongozo mbalimbali."

"Majukumu yako kwa mujibu wa sheria, shirika lina jukumu kubwa sana katika mafuta na gesi kwa maana mkondo wa juu, mkondo wa kati na chini pia kutekeleza majukumu ya kitaalamu.

"Yakiwemo ya kuweza kuhakikisha kuna uwekezaji mkubwa katika hii sekta. Mpaka sasa tuna futi za ujazo takribani trilioni 57 za gesi iliyogundulika."

"Maeneo mengine ni kwamba tunayo haki ya kipekee katika mkondo wa chini na kati kwenye sekta ndogo ya gesi hususani kuhakikisha kwamba masuala yote ya kulinda masilahi ya Serikali pia kushirikiana na wawekezaji wengine kuendeleza gurudumu hili na kutumia utaalamu wetu katika pia usimamizi wa miundombinu mbalimbali."

"Bodi yetu inafanya kazi, imejipanga katika muundo wa kamati kubwa nne ambazo zinahusika na mambo mbalimbali ikiwemo afya,usalama na mazingira na ustawi katika dhana nzima ya uendeshaji wa shirika na sekta kwa ujumla.

"Na pia kamati nyingine ambayo inahusika na uwekezaji na biashara zinazofanywa na shirika."Shirika lina mipango yake ambayo ni pamoja na utelekezaji wa miradi mikubwa ya kitaifa, kwa sasa shirika ni moja kati ya wadau muhimu katika utekelezaji wa LNG ambao unakadiriwa kuwa na thamani ya dola Bilioni 42 kwa mujibu wa hesabu za sasa.
"Lakini ni washirika, Serikali kwa asilimia 15 katika bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki, lakini tuko katika uendelezaji wa kitalu huko Ruvuma.

"Pia tuko kwenye utafutaji na utafiti mbalimbali katika maeneo ya Wembere,Songosongo Magharibi ambako kumeonekana kuna potential resource ya kuweza kuvuna.

"Eyasi Wembere tumeweza kuwa na viashiria vizuri vya mafuta,lakini Songosongo ni katika masuala ya gesi asilia vile vile tunashiriki katika utengenezaji wa miundombinu na hii inafanywa zaidi kupitia kampuni tanzu ya GASCO.

"Lakini pia tuko katika biashara ya mafuta ambayo inasimamiwa na TANOIL tunashirikiana na TPDC na pia kuna miradi mingine ambayo inaendelea kupangwa."

"Ni pamoja na mradi wa CNG kwa ajili ya matumizi ya magari na kuendelea, sehemu ya miradi hii iko katika miradi kielelezo ya mpango wa tatu wa maendeleo ya taifa ya miaka mitano 2021/2022 mpaka 2025/2026 na lengo ni kwamba katika hii miradi 17 miradi minne iko Wizara ya Nishati.

"Na miradi mingine iko TPDC na TPDC jukumu kubwa ni kufanikisha hii ikiwa ni utekelezaji wa ibara ya 63 ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020."

"Ambayo inazungumza nia na dhamira dhabiti ya kuhakikisha kwamba miradi ya nmna hii inatekelezeka nchini na pia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Bunge la 12 alifafanua wazi kusudio lake, 

"Miradi hii ni kutekeleza ikiwemo mradi huu wa LNG, majadiliano yakamikike na mradi uweze kutekelezeka na jukumu kubwa limewekwa TPDC.

"Uhusiano wa TPDC na kampuni tanzu upo katika nyaraka mbalimbali, lakini hapa tumegawanya mafungu mawili la kwanza uhusiano ambao umetamkwa kwa mujibu wa sheria.
"Tunazo sheria mbalimbali zinazosimamia mahusiano ikiwepo sheria iliyoanzisha mashirika ya umma, sheria ya petroli inayotambua baadhi ya majukumu, sheria ya makampuni inayotambua share holders pia Sheria ya Msajili wa Hazina pia imetoa wajibu."

"Kikubwa pia tunazo katiba za makampuni zinazoeleza majukumu ya wanahisa pamoja na majukumu ya menejimenti katika usimamizi na utendaji wa makampuni pia kwa sasa tunaendelea kupata miongozo."

"Nafasi ya kampuni tanzu ni kubwa kwa sababu ni kama uwekezaji wa shirika, kupitia kampuni tanzu ni nyenzo muhimu katika utekelezaji kwa GASCO wanalenga kuimarisha miundombinu, 

"Matengenezo na kufanya mambo mengine yenayoweza kuleta faida. TANOIL yenyewe ni kuimarisha biashara na kuhakikisha kuna uhakika wa bidhaa za mafuta nchini endapo itatokea shortage,"amefafanua kwa kina Dkt.Elias.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news