Global Fund imeimarisha Sekta ya Afya nchini-Dkt.Yonazi

DAR ES SALAAM-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameupongeza na kuushukuru Mfuko wa Dunia (Global Fund) kwa mchango mkubwa unaoutoa katika kuendeleza mapambano dhidi ya magonjwa ya UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu nchini. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Uundwaji wa Miradi ya Mfuko wa Dunia (Global Fund) kwa kipindi cha mwaka 2024- 2026 uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Ametoa pongezi hizo wakati akifungua mkutano wa Uundwaji wa Miradi ya Mfuko wa Dunia (Global Fund) kwa kipindi cha mwaka 2024- 2026 uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya APC Bunju Dar es Salaam.

Mkutano huo ulioudhuriwa na wajumbe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Sekretarieti ya TNCM, Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Pamoja na Asasi za Kiraia. 
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Uundwaji wa Miradi ya Mfuko wa Dunia (Global Fund) kwa kipindi cha mwaka 2024- 2026 wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.

Akieleza kuhusu mchango wa Mfuko wa Dunia katika sekta ya afya nchini, Dkt. Yonazi alisema kuwa, nchi imeendelea kupiga hatua kwa kuzingatia ufadhali wanaoutoka kwa lengo la kugharamia miradi ya Malaria, Kifua Kikuu, UKIMWI na Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji wa Huduma za afya.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Uundwaji wa Miradi ya Mfuko wa Dunia (Global Fund) kwa kipindi cha mwaka 2024- 2026 wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.

“Nchi yetu imepiga hatua kubwa katika kupambana na magonjwa ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria kupitia ushirikiano thabiti na misaada mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Mfuko wa Dunia yaani Global Fund,"alisisitiza.
Mkuu wa Program Wizara ya Afya Dkt. Catherine Joachim akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.

Aidha, alisema kuwa Tanzania bado ni miongoni mwa nchi zinazokumbwa na changamoto za magonjwa hayo na yameendelea kusababisha vifo kwa wananchi walio wengi hali inayopelekea kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Mratibu wa Mfuko wa Dunia kutoka Wizara ya Fedha Bi. Mukajungu Kamuzora akizungumza kuhusu utayari wa wizara yake katika kuhakikisha usimamii wa matumizi ya fedha katika mapambano Dhidi ya magonjwa ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria, wakati wa mkutano Uundwaji wa Miradi ya Mfuko wa Dunia (Global Fund) kwa kipindi cha mwaka 2024- 2026 uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Alitumia jukwaa hilo kuwaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya.

“Ushirikishwaji wa Wadau Watekelezaji wa Nje ya Serikali (PR2) katika mapambano haya ni kipaumbele cha Serikali yetu. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mtendaji wa Tanzania Natioanal Coordinationg Mechanism (TNCM) Dkt. Rachel Makunde (katikati) pamoja na Mratibu wa Mfuko wa Dunia kutoka Wizara ya Fedha Bi. Mukajungu Kamuzora (wa kwanza kulia) wakifuatilia mkutano huo.

"Niwaombe wadau wetu kwa pamoja tushirikiane kufikisha huduma hizi katika jamii yote inayotuzunguka.Ninawasihi muendelee kushirikiana na Serikali katika kuleta uzoefu hususan pale tunapohitajika kuongeza ufanisi na tija katika miradi na huduma za afya,”alisema Dkt.Yonazi.
Katibu Mtendaji wa Tanzania Natioanal Coordinationg Mechanism (TNCM) Dkt. Rachel Makunde akizungumza wakati wa Mkutano wa Uundwaji wa Miradi ya Mfuko wa Dunia (Global Fund) kwa kipindi cha mwaka 2024- 2026 Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tanzania Natioanal Coordinationg Mechanism (TNCM) Dkt. Rachel Makunde alimshukuru Katibu Mkuu ambaye pia ni mwenyekiti wa TNCM kwa usimamizi wake na mchango anaoutoka katika kuyafika malengo ya chombo hicho.

Naye Dkt. David Sando, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la MDH aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa Program hizo ili kuimarisha huduma za afya nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la MDH, Dkt. David Sando akieleza mikakati ya shirika lake katika kuendeleza jitihada za mapambano dhidi ya magonjwa ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria wakati wa mkutano huo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

“Tumeendelea kusupport zaidi ya wagonjwa laki tatu wanaotumia dawa za kufubaza Makali ya Virusi vya UKIMWI (ARVs) na kupitia miradi ya HIV, tumeweza kuwafikia wagonjwa wengi katika mikoa 12 tunayoihudumia ambapo ni zaidi ya nusu ya wagonjwa wote nchini,” alieleza Dkt. Sando.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news