Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia washiriki Maonesho ya Mwaka ya Kibiashara ya Ongwediva

Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia, Bi. Upendo Mwasha (kushoto) akimwonesha mteja vazi aina ya batiki kutoka Tanzania wakati wa Maonesho ya Mwaka ya Kibiashara ya Ongwediva ambayo yanafanyika nchini humo kuanzia tarehe 27 Agosti, 2023. Maonesho hayo ambayo yalifunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Namibia, Mhe. Verna Sinimbo yamewashirikisha Wajasiriamali kutoka Tanzania na Diaspora wanaoishi nchini Namibia. Mbali na kuonesha bidhaa mbalimbali za Tanzania, Ubalozi umetumia maonesho hayo kutangaza Lugha ya Kiswahili kwa kuweka vitabu vya kiswahili katika Banda la Ubalozi na kuhamasisha wateja kusoma na kujifunza Lugha hiyo kupitia Ubalozi ambao umeanzisha Maktaba ya Kiswahili. 
Wadau mbalimbali wakitembelea Banda la Tanzania kwenye maonesho hayo.
Baadhi ya Wajasiriamali wa Tanzania wakishiriki maonesho ya Mwaka ya Kibiashara ya Ongwediva yanayofayika nchini Namibia.
Banda la Tanzania kama linavyoonekana pichani. Bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania zinazooneshwa kwenye maonesho hayo ikiwa ni pamoja na nguo za batiki, vikapu, viatu vya asili, shanga, kahawa na majani ya chai.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news