Rais Dkt.Samia awapa kongole wakulima, wavuvi na wafugaji

MBEYA-Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kukutana mapema leo jijini Mbeya, katika kilele cha Maonesho ya Thelathini ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane).

Nawapongeza mamilioni ya wakulima, wavuvi na wafugaji katika kila kona ya nchi yetu kwa juhudi zenu katika uzalishaji, na kuendelea kulilisha Taifa letu.

Kazi zenu za kila siku zinaipa nchi yetu si tu uhakika wa chakula lakini pia ajira (zaidi ya asilimia 65), malighafi kwa viwanda vyetu (zaidi ya asilimia 60), na zinachangia zaidi ya robo ya Pato la Taifa letu.

Tumeongeza Bajeti katika Kilimo lakini pia katika Mifugo na Uvuvi ili tutekeleze mipango tuliyojiwekea katika sekta hizi muhimu kwa uchumi na maisha ya kila Mtanzania.

Nazipongeza Wizara zote mbili kwa programu nyingi bora na mahususi zinazoendelea kutekelezwa. Programu mojawapo ni Jenga Kesho Iliyo Bora, inayowapa vijana na wanawake mafunzo ya kilimo, umiliki wa ardhi kwa zaidi ya miaka 66 na nafasi ya masoko ya mazao yao.

Kwa namna ya kipekee, Serikali itaendelea kutoa ruzuku katika mbolea na pembejeo. Nimeagiza Wizara ya Kilimo kukaa na Wizara ya Fedha ili kuondoa gharama za kusambaza mbolea kwa ngazi ya kata ambazo zinafanya bei ya mboleo kwa mkulima kuwa juu.

Imeandikwa na,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan
Leo Agosti 8, 2023

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news