Rais Dkt.Samia awataka mabalozi kutafuta fursa

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka Mabalozi kufuatilia utekelezaji wa Mikataba na Hati za Makubaliano zinazotokana na ziara za viongozi ndani na nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kamishna wa Maadili Jaji Mhe. Sivangilwa Mwangesi kwenye picha ya kumbukumbu na Mabalozi Wateule aliowaapisha kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.

Rais Samia ametoa tamko hilo leo Agosti 16,2023 katika hafla ya kuwaapisha Mabalozi wateule iliyofanyika Ikulu,Chamwino jijini Dodoma. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi, Mabalozi Wateule pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.

Aidha, Rais Samia amesema ufuatiliaji huo uende sambamba na utekelezaji wa makubaliano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali yanayotokana na Tume za Pamoja za Ushirikiano na Mashauriano ya Kidiplomasia.
Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023. 

Vile vile, Rais Samia amewataka Mabalozi kuibua masuala ya ushirikiano katika vituo vyao vya kazi na kutafuta fursa mbalimbali ikiwemo katika sekta ya uwekezaji, utalii pamoja na mahitaji ya ‘diaspora’. 

Rais Samia pia amewataka Mabalozi kufanya kazi kwa kuzingatia Dira ya Ajenda za Maendeleo za kimataifa na kitaifa ikiwemo falsafa ya 4Rs (Maridhiano, Ustahamilivu,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli, kuwa Balozi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.
Mabalozi Wateule wakila Kiapo cha Maadili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.
Mabalozi Wateule wakisaini Hati za kiapo cha Maadili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.

Mabadiliko na Kujenga Upya) kwa maslahi ya taifa.Kwa upande mwingine, Rais Samia ameielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inaandaliwa mfumo utakaoingiza maelekezo ya ziara za viongozi wa ndani na nje ya nchi.

Rais Samia ameongeza kuwa mfumo huo utaonesha jukumu la kila wizara kwenye makubaliano yaliyofikiwa ili kuweza kupima utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news