Tangazeni mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita-Dkt.Mabula

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),MNEC Dkt. Angeline Mabula amewataka wanachama wa chama hicho kutangaza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ili yaweze kufahamika kwa wananchi. 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Angeline Mabula akiwasili ofisi za CCM Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe wakati wa ziara yake mkoani humo. Kulia kwa Dkt.Mabula ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba.

Dkt.Mabula ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema hayo Agosti 11, 2023 alipotembelea ofisi ya CCM Wilaya ya Ludewa na kuzungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho akiwa katika ziara yake Mkoa wa Njombe. 

Alisema, wakati Serikali ya Awamu ya Sita ikifanya mambo makubwa ya kuwaletea watanzania maendeleo, viongozi pamoja na wanachama wa CCM katika ngazi mbalimbali wana jukumu la kutangaza mafanikio yaliyofanywa na serikali inagoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan. 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Angeline Mabula akizungumza kwenye kikao na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ludewa, Stanley Kolimba na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva. 

"Chama kitangaze mafanikio ya serikali na ninyi viongozi wa ngazi mbalimbali mnalo jukumu hilo ambapo Rais wetu Samia Suluhu Hassan ameonesha kuwajali wananchi kwa ujenzi wa madarasa, zahanati pamoja na kuanzizsha shule mpya, hayo ni mafanikio makubwa,"alisema Dkt.Mabula. 

Kwa mujibu wa Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, yote yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kiasi kikubwa yamemgusa kila mtu kutokana na kulenga huduma za jamii. 
Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wakimpokea Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Dkt.Angeline Mabula alipotembelea ofisi za chama hicho. 

Dkt.Mabula pia amegusia miradi mikubwa ya kimkakati kama vile Bwawa la Mwalimu Nyerere pamoja na reli ya mwendo kasi kuwa ni miradi inayokwenda kuipaisha Tanzania ambapo amesema, hata mchakato wa bandari unaoendndelea sasa utakapokamilika unaenda kuwa wa aina yake. 

Aidha, amekitaka Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa kuangalia fursa za uwekezaji katika miradi mbalimbali na kutolea mfano wa Liganga na Mchuchuma kuwa chama kinaweza kuwekeza katika eneo hilo ili kukiwezesha kutekeleza majukumu yake bila kutegemea misaada. 
Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Dkt.Angeline Mabula alipotembelea ofisi za chama hicho wilayani Ludewa. 

"Ni vizuri chama kikaangalia fursa zinazopatikana, kama hapa mnao mradi wa Liganga na Mchuchuma mnaweza kuomba vitalu na kuwekeza ili chama kiwe na nguvu na kujisimamia chenyewe jambo litakalowafanya kuheshimika na kama huwezi kujisimamia siyo vizuri,"alisema Dkt.Mabula. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news