Waziri Dkt.Gwajima awakabidhi Simba SC Kombe la Ngao ya Jamii

TANGA-Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amekabidhi Kombe la Ngao ya Jamii kwa Klabu ya Simba mara baada ya klabu hiyo kuibuka mshindi katika mchezo wa fainali ya ngao ya jamii dhidi ya klabu ya Yanga Agosti 13, 2023.
Mashindano hayo ya ngao ya jamii yamewezesha pia kuinua sauti ya wito kwa jamii kupambana kutokomeza ukatili kwa watoto ambapo Wizara ikishirikiana na TFF na Vilabu vya Yanga, Simba SC, AZAM FC na Singida Fountain Gate imetoa elimu kuhusu umuhimu wa kuwalinda watoto.

Waziri Dkt. Gwajima ametumia nafasi hiyo akizungumza na vyombo vya habari jijini humo, kutoa wito kwa vilabu vingine vyote kushiriki kampeni ya kuwalinda watoto kupitia ligi kuu itakayoanza hivi karibuni.

Katika mchezo huo, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameambatana na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Sebastian Kitiku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news