OUT yarejesha tabasamu kwa wenye mahitaji maalumu Mwanza

MWANZA-Jamii ya Watanzania imeaswa kuendelea kutoa huduma kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kuwawezesha kutimiza ndoto zao katika maisha.
Hayo yamesemwa na Prof. Elifas Tozo Bisanda Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) wakati wa hafla ya utoaji wa mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya sekondari Mkolani iliyofanyika tarehe 10/08/2023 katika shule hiyo ya jijini Mwanza.

"Chuo chetu ni miongoni mwa taasisi za Umma ambazo zipo msitari wa mbele katika kutoa mchango wa hali na mali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum hapa nchini. 

"Pale Kinondoni tunatoa mafunzo bure ya matumizi ya TEHAMA kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu." 
Akizungumzia hafla hiyo, Mkurugenzi wa OUT Mwanza Dkt. Ancyfrida Prosper ameeleza kwamba, kituo kimeendelea na juhudi zake katika kutoa huduma kwa jamii ambapo katika shule ya sekondari Mkolani wamefanikiwa kutoa fimbo nyeupe kwa wasioona, sabuni, daftari, taulo za kike, karatasi za rimu, kalamu na mafuta ya kupaka mwili kwa jumla ya wanafunzi 98 wenye mahitaji maalumu katika shule hiyo.

"OUT Mwanza tunaamini kwamba, wanafunzi wenye mahitaji maalumu ni hazina kubwa kwa taifa letu kwani miongoni mwao wapo wenye vipaji mbalimbali. Hivyo wakiwezeshwa wanaweza na wakikumbukwa inawapa hamasa ya kufanya vizuri zaidi katika masomo yao,"amesema Dkt.Ancyfrida.

Kwa upande wake Afisa Elimu Maalum wa Jiji la Mwanza,Bi. Bertha Donald, ametoa shukurani za dhati kwa uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa upendo na kuonesha kuwajali na kuwakumbuka wanafunzi wenye mahitaji maalum. 
"Wanafunzi hao tunawafundisha na wanaweza kuwasiliana asiyeona na asiyesikia, asiyezungumza na asiyeona na kuwawezesha kuwasiliana kikamilifu baina yao na wanajamii wengine kwa jumla. 

"Hivyo, tunachokifanya hapa Mkolani sekondari leo ni muendelezo wa kile ambacho Chuo chetu kimekuwa kikifanya kwa muda mrefu,"Amesema Prof. Bisanda.

Aliendelea kueleza kwamba, mafunzo hayo tunayoyatoa yanawasaidia wenye mahitaji maalum kuweza kutumia mitandao ya kijamii kikamilifu katika mawasiliano na hata kutengeneza ajira na kupata kipato cha kujikimu kimaisha.
"Natoa shukurani za dhati kwako Prof. Bisanda Makamu Mkuu wa Chuo-OUT na timu nzima ya OUT-Mwanza chini ya Mkurugenzi Dr. Ancyfrida kwa upendo wenu mkubwa kwa watoto hawa. 

"Hakika mmefanya jambo kubwa ambalo litawatia hamasa wanafunzi hawa kufanya vizuri katika masomo yao. 
"Natoa rai kwa taasisi nyingine za umma na binafsi na pia kwa wanajamii mmojammoja kuiga mfano wa OUT katika kuwajali wanafunzi wenye mahitaji maalum."

Hafla hiyo ya utoaji wa huduma kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ni moja ya shughuli zilizoambatana na kuipamba Wiki ya Utumishi wa Umma kwa OUT inayofanyika kuanzia tarehe 7 mpaka 14 Agosti,2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news