Kamchape wayakanyaga mkoani Katavi

KATAVI-Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, linaendelea na zoezi la utoaji wa elimu kwa jamii, ili iweze kuachana na vitendo vya imani za kishirikina, ramli chonganishi na matukio mbalimbali ya kiuhalifu.
Hatua hiyo, imefikiwa baada ya kuibuka kwa vitendo vya upigaji wa ramli chonganishi vinavyofanywa na kikundi cha kihalifu cha Kamchape au Lambalamba.

Hali inayopelekea uwepo wa taharuki na makosa ya jinai ya kujeruhi, kuchoma nyumba na mazao moto pamoja na uharibifu wa Mali. 

Aidha,kufuatia hali hiyo Septemba 15 na 16, 2023 Polisi ilifanya oparesheni ikiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, ACP Kaster Ngonyani, kwa kupiga doria maeneo mbalimbali ya mwambao mwa Ziwa Tanganyika na kufanikiwa kuwakamata watu kadhaa. 

Operesheni hiyo ilipita katika vijiji vya Kapalamsenga, Karema, Mijeti na Ikola na kufanya vikao na viongozi wa vijiji pamoja na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi, ambapo watu hao wanashikiliwa kwa mahojiano, na wanatarajia kufikishwa mahakamani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news