Mbinga DC yawakaribisha wawekezaji

RUVUMA-Kaimu Mkuu wa Idara ya Viwanda, Bishara na Uwekezaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Bi. Martina Ernest Ngahi ametoa wito kwa wawekezaji waliopo ndani na nje ya Mkoa wa Ruvuma kuja kuwekeza katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

Amesisitiza kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ina maeneo na fursa nyingi za kichumi ambazo zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo nchini.

Bi. Martina ametoa wito huo leo Septemba 2, 2023 wakati akizungumza katika kipindi cha radio MBINGA YETU kinachorushwa na Radio Hekima iliyopo katika Wilaya ya Mbinga.

"Katika halmashauri yetu tuna fursa mbalimbali za kiuchumi mfano uwekezaji wa usindikaji wa sembe au zao la soya, ujenzi wa mahoteli na nyumba za kulala wageni na kadhalika,"amesema Bi. Martina

Kipindi cha MBINGA YETU kinarushwa kila Jumamosi kuanzia saa sita mchana hadi saa saba, katika kipindi hiko utapata taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Aidha, Bi. Martina amewakumbusha wafanya biashara waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuwa wabunifu na kutumia changamoto zilizopo kama fursa katika kuanzisha au kuimarisha biashara zao.

"Ukiwa mfanya biashara lazima uwe mbunifu sio unaiga kila biashara jitahidi kupambania na kwenda nje ya boksi."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news