Musoma Vijijini yatoa ratiba ya uchangiaji, uhamasishaji miradi

NA FRESHA KINASA

OFISI ya Mbunge la Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara chini ya Mheshimiwa Prof.Sospeter Muhongo imetoa ratiba ya uchangiaji.

Sambamba na uhamasishaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika vijiji mbalimbali vilivyopo ndani ya jimbo hilo.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo iliyotolewa Leo Septemba 21, 2023 imewahimiza viongozi,Mbunge wa Jimbo,Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM) na viongozi wengine ambao wanakaribishwa kushiriki kikamilifu

Vile vile,Mbunge wa jimbo, Mheshimiwa Prof.Muhongo atasikiliza matatizo na kero za wananchi ambapo ratiba inaanza Septemba 27, 2023 siku ya Jumatano saa 4 asubuhi watakuwa Kisiwa cha Rukuba, Kata ya Etaro kwa ajili ya harambee ya ujenzi wa sekondari.

Septemba 29,2023 siku ya Ijumaa majira ya saa 4 asubuhi watakuwa kijijini Kwikerege, Kata ya Rusoli kwa ajili ya harambee ya ujenzi wa zahanati.

Aidha, siku hiyo hiyo majira ya saa 8 mchana watakuwa kijijini Musanja, Kata ya Musanja kwa ajili ya harambee ya ujenzi wa Shule Shikizi Gomora.

Katika mwendelezo wa ratiba hiyo, Oktoba 2, 2023 siku ya Jumatatu majira ya saa 4 asubuhi watakuwa Kijijini Kurwaki, Kata ya Mugango kwa ajili ya arambee ya ujenzi wa David Massamba Memorial Secondary School.

Siku hiyo hiyo, majira ya saa 8 mchana watakuwa kijijini Nyasaungu, Kata ya Ifulifu kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa sekondari.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,ratiba kwenye kata nyingine itafuata.

"Wazaliwa wa Musoma Vijijini wanaendelea kuombwa na kushawishiwa kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya vijijini kwao."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news