Nay wa Mitego awasili Police Central

DAR ES SALAAM-Staa wa Bongo Fleva,Emmanuel Elibariki Munisi (Nay wa Mitego) amewasili Police Central jijini Dar es Salaam kuitikia wito kuhusu wimbo wake wa Amkeni.

Wimbo huo hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitangaza kuufungia kuchezwa katika vituo vyote vya radio na televisheni nchini.

Kwa mujibu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) walieleza kuwa, maudhui ya wimbo huo wa Rapa Nay wa Mitego yana mwelekeo wa kutaka wananchi wasiwe na imani na Serikali. Pia unachochea mapokeo hasi juu ya utekelezaji wa mipango ya Serikali kwa ujumla.

Aidha, Rapa huyo ambaye amewasili akiwa na Mwanasheria wake Jebra Kambole amenukuliwa akisema kuwa, “Ukiwa sauti ya watu kuja sehemu kama hii ni kawaida.

"Mimi ni sauti ya watu, acha nikawasikilize, nitakuwa na cha kuongea, lakini kwa sasa sina, nimeambiwa tu ni wimbo wangu wa Amkeni, kwa hiyo nataka nikajue umefanya nini, kuna tatizo gani,"amesema Msanii huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news