Spika Dkt.Tulia ateta na Spika wa Morocco

RABAT-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Spika wa Bunge la Morocco, Mhe. Rachid Talbi El Alami katika ofisi za Bunge hilo zilizopo jijini Rabat nchini Morocco leo Septemba 18, 2023.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Mabunge ya nchi hizo mbili hususani katika sekta ya kilimo, viwanda na biashara.

Aidha, Dkt.Tulia ametumia nafasi hiyo kutoa pole kwa Serikali ya Morocco kwa vifo vya watu zaidi ya 3000 na madhara yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo mapema mwezi huu.

Pia amepongeza juhudi zilinazofanywa na Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco katika kukabiliana na maafa pamoja na changamoto zilizotokana na tetemeko hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news