Tabora United FC yaichapa Tanzania Prisons mabao 3-1

TABORA-Timu ya Tanzania Prisons imepoteza mchezo wa pili mfululizo dhidi ya Tabora United FC kwa mabao 3-1.

Ni kupitia mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambao umepigwa Septemba 15, 2023 katika Dimba la A;lly Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Tabora United iliyopoteza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Azam FC kwa mabao 4-0, imepata ushindi huo wa kwanza kwa mabao ya John Ben aliyefunga mawili dakika ya 42 na 90 na Erick Okutu dakika ya 58.

Aidha, kupitia mtanange huo, bao la Tanzania Prisons limefungwa na Samson Mbangula dakika ya 70 ya mchezo huo.

Prisons imeruhusu mabao sita kwenye michezo miwili iliyopita huku wakiwa na alama moja pekee waliyopata suluhu dhidi ya Singida Fountain Gate inayowaweka nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Wakati huo huo, Tabora United FC maarufu kama Nyuki wa Tabora inafikisha alama nne. Katika mtanange huo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mhe.Balozi Dkt.Batilda S Burian alifika kuwapa hamasa vijana wake.

Aidha, baada ya matokeo hayo, Mheshimiwa Balozi Dkt.Burian aliwapatia vijana hao fungu la fedha kwa ajili ya kuunga mkono jitihada zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news