Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Italian Shipping Academy waingia makubaliano

ROME-Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Chuo cha Italian Shipping Academy kilichopo nchini Italy ya kubadilishana uzoefu katika mafunzo ya ubaharia na kushirikiana katika tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy (FAIMM), Eugenio Massolo wakionesha Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo ya ubaharia na tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu katika hafla iliyofanyika jijiNI Roma, Italy.

MOU hiyo imesainiwa nchini Italy na Dkt.Tumaini Gurumo, Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy (FAIMM) Bw. Eugenio Massolo.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha DMI, Dkt. Tumaini Gurumo amesema kuwa makubalino hayo ya miaka mitano yatasaidia kuongeza ujuzi kati ya Wanafunzi na Wahadhiri kwa pande zote mbili.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo wakipongezana baada ya kusaini MOU ya kushirikiana katika mafunzo ya ubaharia, tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu katika hafla iliyofanyika jijini Roma, Italy.

“Nimefurahi sana kuingia Makubaliano haya kwakua wenzetu wapo tayari kushirikiana nasi katika miradi mbalimbali, ninaona ndoto ya kufikia viwango vinavyokubalika na EU inakwenda kutimia,"alisema Dkt.Tumaini.

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Balozi Tanzania nchini Italy Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Italy nchini Tanzania Mhe. Marco Lombardi.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo wakionesha Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo ya ubaharia na tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu katika hafla iliyofanyika jijini Roma, Italy.

Kwa upande wake Balozi Kombo amesema kuwa Italy imepiga hatua katika teknolojia hivyo utayari wao wa kushirikiana na DMI utaiwezesha zaidi Tanzania kukua katika eneo hilo. Vilevile Balozi Kombo ametoa wito kwa upande zote mbili kuteleza vipengele vya makubaliano ipasavyo ili izae matunda yanayotarajiwa.

Naye Mkuu wa Chuo cha Italian Shipping Academy Foundation (FAIMM) Eugenio Massolo amesema kuwa makubaliano hayo yatasidia kukuza ujuzi kwa pande zote mbili ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news