Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya yazindua jengo la kutolea huduma ya tiba mazoezi

MBEYA-Katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imezindua jengo jipya la kutolea huduma ya Tiba Mazoezi (Fiziotherapia) kwa ajili ya kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma hiyo kwa wagonjwa wenye matatizo ya maumivu ya viungo.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa Jengo hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji ameushukuru uongozi wa hospitali pamoja kamati yote iliyofanikisha kukamilika kwa jengo hilo pamoja na ushirikiano ulioonyeshwa na watumishi wa hospitali akiwemo Mhandisi alisiyesimamia shughuli zote za ujenzi huo.

“Shukrani zote nilizopewa ni za uongozi wa hospitali na watumishi wote kwa sababu vyote vilivyofanyika ni watumishi wamefanya kazi kupitia sehemu ya mapato yanayopatikana,"amesema Dkt.Mbwanji.

Aidha, Dkt. Mbwanji ametoa rai kwa watumishi wa idara hiyo inayohusika na huduma ya Tiba mazoezi kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa yasiyo ya lazima.

Naye Mkuu wa Idara ya Fiziotherapia, Seraphine Mushi ameushukuru uongozi kwa kupitia maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika idara hiyo ikiwemo ongezeko la vifaa tiba pamoja na upanuzi wa jengo hilo ambapo hapo awali lilikuwa na uwezo kuhudumia wagonjwa wa nje 30 hadi 40 kwa siku na sasa lina uwezo wa kuhudumia wagonjwa wa nje zaidi ya 120 hadi 200 kwa siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news