Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanawake U20 amshukuru Mungu

DAR ES SALAAM-Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanawake U20 (Tanzanite), Ester Chabruma amemshukuru Mungu kwa ushindi mnono dhidi ya Djibouti.

Akizungumza baada ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Djibouti uliomalizika kwa Tanzania kupata ushindi wa magoli 5-0, Chabruma amesema;

"Kwanza, tunamshukuru Mungu kwamba mechi yetu imeisha, matokeo tumeyapokea vizuri, kwa maana tumepata magoli mengi na watu wamecheza tumeona, kwa hiyo tunamshukuru sana Mwenyenzi Mungu.

"Ni kweli, tuna siku mbili lakini,kubwa yote kwa yote tutakachokifanya tutaangalia wapi penye mapungufu turekebishe na yale mazuri tuyaongeze zaidi ili tuje kufanya vizuri katika mechi inayofuata.

"Cha kwanza haya ni mashindano, wenzetu wamejiandaa kulingana na masdhindano yalivyo na sisi tumejiandaa kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mashindano.

"Lakini cha kwanza tunamshukuru Mwenyenzi Mungu, tumefanya vizuri kwenye mechi yetu ya kwanza na tutapambana kuhakikisha mechi ya pili tunapata ushindi ili tuweze kufanya vizuri zaidi,"amefafanua Kocha huyo.

Mtanange huo umepigwa Oktoba 8, 2023 katika Uwanja wa Azam Complex katika Kata ya Chamanzi uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Jamila Rajab ndiye alitupia mawili nyavuni, Noela Luhala,Winfrida Gerlad na Yasinta Joseph wakamalizia ushindi huo.

Aidha,timu hizo zitarudiana Jumatano hapo hapo Azam Complex Djibouti akiwa mwenyeji na mshindi wa jumla atakutana na Nigeria katika Raundi ya Tatu ya mbio za nchini Colombia 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news